Tumia muda wako kunijua.
Nisikilize na uniruhusu nijitoe kwako.
Ninakupa muda wa kuutumia.
Ninakupa muda ili ufurahie.
Uwe na amani kuhusu zawadi hii.
Elekeza matumizi ya zawadi yako ya muda
kwa mwongozo ninaokupa.
Sikiliza maneno ninayokuambia kupitia wengine.
Pokea maneno haya ya hekima kutoka Kwangu
na utumie ufahamu huu kuongoza matumizi ya muda wako wa thamani.
Usijaribu kuelewa mambo yote,
kwa maana utachoka kwa juhudi hizo.
Uwe tayari kuyaamini maneno ya hekima
unayopewa.
Acha hali yako ya kutoamini
ambayo haikuongozi kunielekea Mimi.
Sitakudhuru.
Nitumainie kama mtoto wa kike anavyowatumainia mama yake na baba yake.
Niruhusu nikuongoze.
Niruhusu nikusaidie.
Niruhusu nikubariki.
Niruhusu nikuponye hali ya kutoamini.
Niruhusu niwe na muda wako.
Ukifanya hivi,
nitakupa yote yenye baraka
na usiyoyajua.
