Unatafuta kisichojulikana
lakini hukipati.
Nitafute Mimi
na upate unachokitafuta.
Unapata furaha gani
katika unayoyafanya?
Unapata heri gani
katika ulicho nacho?
Ni amani gani inayotokana
na matukio na matamanio haya.
Elekeza hamu yako Kwangu
na upate amani yako.
Elekeza matumaini yako Kwangu
na ugundue maisha yako ya baadaye.
Nigeukie kwa moyo wako
na uone ninachokutakia.
Jielekeze Kwangu
na upate furaha inayokungoja.
Weka hofu yako kando
na badala yake uwe na matumaini.
Ondoa akilini mwako
yale yanayokuzuia kuja Kwangu.
Weka mzigo wako mikononi Mwangu,
nami nitakuondolea.
Leta mashaka yako Kwangu,
kwa maana yatakupofusha.
Kipofu hawezi kuona
kwa kukosa uwezo wa kuona.
Kizuizi hiki kinapoondolewa,
anaweza kuona.
Upofu wako unapoondolewa,
unaweza kuona.
Una vizuizi gani vinavyokuzuia kuona?
Unaponitafuta Mimi,
unapata nini?
Je, upofu wako hukufanya uone isivyo kweli?
Unapouona mkono Wangu ukitenda kazi,
unaniona Mimi kwa namna gani?
MIMI NDIMI kile unachokitafuta.
