Ni matumaini gani yaliyopo isipokuwa matumaini Yangu?
Ni faraja gani iliyopo
isipokuwa faraja Yangu?
Ni upendo gani ulio na nguvu kuliko Wangu?
Hata pumzi moja ya hewa haina maana
bila mwongozo Wangu.
Hata dakika moja ya siku yako haina thamani
bila maelekezo Yangu.
Fuata njia Yangu na uone njia yako.
Tafuta namna Zangu za kutenda na uelewe unakoelekea.
Yapokee maneno Yangu na utambue mpango Wangu.
Hakuna hata sekunde moja inayopita
bila wewe kuwa mbele ya macho Yangu.
Mimi nimo ndani yako daima.
Tafuta uwepo Wangu
na ujue kwamba niko pamoja nawe.
Itambue asili Yangu
na ujue kwamba ninakujali.
Acha asili Yangu ikumbatie muda wako
ili ikuletee uradhi
na kuridhika kila siku inayopita.
