Unaona nuru gani
unapotafuta majibu usiyoyajua?
Je, majibu yako hayatoshi
kukidhi hamu yako ya kuelewa?
Je, unachanganyikiwa
na tafakuri zako na hali yako ya kutotulia?
Tambua kwanza kutoweza kwako
kujibu maswali ya maisha.
Fahamu kwamba ni kidogo tu
kinachotarajiwa kwako.
Ikiwa unabeba mzigo mzito,
basi uachilie.
Uinuliwe,
unapoitambua nuru Yangu.
Furahia joto lake na fadhili zake.
Utiwe moyo na mguso wake.
Acha nuru Yangu ikujaze
kwa yale usiyoyajua.
Ruhusu hili.
Omba hili.
Tarajia hili.
