Utangulizi wa Tafakari za Kipindi cha Mwaka
- Ubatizo wa Bwana
- Bendera Mbili
- Makundi Matatu ya Watu
- Majaribu
- Kuitwa kwa Mitume
- Arusi ya Kana
- Kusafisha Hekalu
- Hotuba ya Mlimani
- Kuituliza Dhoruba
- Kutembea Juu ya Maji
- Mitume Walitumwa Kuhubiri
- Kuongoka kwa Maria Magdalena
- Jinsi Kristo Alivyowalisha Watu Elfu Tano
- Kugeuka Sura kwa Kristo
- Kufufuka kwa Lazaro
- Karamu ya Jioni huko Bethania
- Njia Tatu za Unyenyekevu
Kinapatikana kama kitabu chenye jalada laini na kitabu cha kielektroniki:
Amazon – Google Play– iTunes – Barnes & Noble
Utangulizi
Tafakari kumi na saba katika sehemu hii zitatumika katika nyakati mbili za mwaka tunapokuwa katika Kipindi cha Mwaka. Tafakari nyingi za sehemu hii zimetoka katika “Juma la Pili” la Mazoezi ya Kiroho.
Kwanza, baada ya kumalizika kwa Kipindi cha Noeli, anza na Sikukuu ya Ubatizo wa Bwana, ambayo huchukua nafasi ya Jumapili ya Kwanza ya Kipindi cha Mwaka. Urefu wa sehemu hii ya Kipindi cha Mwaka hutofautiana kila mwaka kutegemea Jumatano ya Majivu inaangukia lini. Kwa hiyo, utatumia tafakari chache tu kati ya hizi katika sehemu hii ya Kipindi cha Mwaka kabla ya Kwaresima.
Tafakari zilizobaki katika sehemu hii zitumike baada ya Kipindi cha Pasaka kuhitimishwa kwa maadhimisho ya Sherehe ya Pentekoste. Hivyo, tafakari zilizobaki katika sehemu hii zitatumika Kipindi cha Mwaka kitakapoanza tena. Ukimaliza tafakari zote mwishoni mwa majira ya kiangazi au mwanzoni mwa majira ya mapukutiko, katika sehemu ya baadaye ya Kipindi cha Mwaka, jisikie huru kurudia baadhi ya tafakari zilizokugusa zaidi katika mwaka mzima.
