Somo la Maandiko Matakatifu: Luka 7:36–50
Muktadha: Simoni, Farisayo, alimwalika Yesu nyumbani kwake kwa chakula cha jioni. Ilikuwa desturi ya ukarimu kuwapokea wageni kwa busu, kuwapaka mafuta kichwani na kuwapa maji ya kunawa miguu walipofika. Simoni hakumfanyia Yesu jambo lolote kati ya hayo ya ukarimu.
Hata hivyo, simulizi hili halilengi sana kulalamikia ukosefu wa ukarimu wa Simoni, bali linaangazia wema wa dhati wa mwanamke huyu aliyetubu. Yesu anaeleza kwamba amesamehewa kwa sababu “amependa sana.” Hivyo, upendo wake na msamaha wenye huruma wa Yesu ndivyo kiini cha simulizi hili.
Simulizi hili pia linaonyesha kwamba Simoni ana tabia ya kuwahukumu wengine sana. Yesu anasoma mawazo yake na kumkemea kwa upole kwa kukosa upendo, lakini anamheshimu mwanamke huyo kwa upendo wake wa kina.
Tafakari: Soma kifungu cha Maandiko Matakatifu hapo juu kwa moyo wa sala na utumie mambo haya ya kutafakari ikiwa yatakusaidia katika tafakari yako:
- Vuta taswira ya Yesu akiwasili nyumbani kwa Simoni. Zingatia ukosefu wa ukarimu. Jaribu kumwazia Simoni.
- Tafakari ujasiri wa mwanamke huyu mwenye dhambi. Mfikirie jinsi ambavyo bila shaka alikuwa na wasiwasi kuhusu kuja karamuni bila kualikwa. Zingatia hofu alizopaswa kuzishinda.
- Jaribu kuchungulia moyoni mwake macho yake yalipokutana na ya Yesu kwa mara ya kwanza. Wazia hisia za ndani zilizomsukuma kuinama hadi chini, kuibusu miguu Yake, kumpaka manukato yake na kulia bila kujizuia.
- Chungulia moyoni mwa Yesu. Ona huruma Yake na jinsi anavyomjali kwa dhati.
Tafakari maneno haya: “Dhambi zako zimesamehewa.” Na “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.”
Picha Kuu: Rubens-Karamu ya Simoni Farisayo
Utangulizi wa Tafakari za Kipindi cha Mwaka
- Ubatizo wa Bwana
- Bendera Mbili
- Makundi Matatu ya Watu
- Majaribu
- Kuitwa kwa Mitume
- Arusi ya Kana
- Kusafisha Hekalu
- Hotuba ya Mlimani
- Kuituliza Dhoruba
- Kutembea Juu ya Maji
- Mitume Walitumwa Kuhubiri
- Kuongoka kwa Maria Magdalena
- Jinsi Kristo Alivyowalisha Watu Elfu Tano
- Kugeuka Sura kwa Kristo
- Kufufuka kwa Lazaro
- Karamu ya Jioni huko Bethania
- Njia Tatu za Unyenyekevu
