Kiswahili

Kugeuka Sura kwa Kristo

Mpangilio wa Saa Takatifu

Somo la Maandiko Matakatifu: Mathayo 17:1–13

Muktadha: Muda mfupi kabla ya kifungu hicho hapo juu, Yesu alitenga wakati wa kuwafundisha wanafunzi Wake kwamba angeteswa, angekufa na kufufuka siku ya tatu. Pia aliwaambia, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake na kunifuata” (Mathayo 16:24b, RSV-CE).

Siku sita baadaye, Yesu anawachukua watatu kati ya wanafunzi hao na kupanda nao mlima mrefu. Ni huko mlimani ambapo hao watatu wanapata ufunuo wenye nguvu wa Yesu alivyo katika utukufu Wake. Musa na Eliya wanamtokea, na Yesu Mwenyewe anageuka sura mbele ya wanafunzi, hata mavazi Yake yanakuwa “meupe kama nuru.”

Musa na Eliya wanawakilisha utimilifu wa Sheria na manabii wa Agano la Kale. Nayo sauti ya Baba inasema, ikimfunua Yesu kuwa Sheria mpya na Nabii mpya. Baba anasema maneno yaleyale aliyosema wakati wa ubatizo wa Yesu, akiongeza tu maneno “msikilizeni Yeye.” Yesu si Sheria mpya na Nabii mpya tu, bali pia ni Neno linalosemwa.

Tukio hili linawapa nguvu na matumaini wanafunzi ambao yaelekea walikuwa wakihangaika kuelewa na kukubali kwamba Yesu angekufa karibuni na kwamba ingewabidi kufuata nyayo Zake, nao wenyewe wakifa. Kwa kuona mwanga huu wa umungu Wake, na kwa kuelewa kwamba Yeye ndiye utimilifu wa Agano la Kale, hawa ambao wangekuwa Mitume waliimarishwa ili kutimiza utume walioitiwa.

Tafakari: Sasa soma tena kifungu hicho hapo juu polepole na kwa moyo wa sala, na uwe huru kutumia mambo yafuatayo ikiwa yatakusaidia.

  • Anza kwa kutafakari siku sita baada ya wanafunzi kumsikia Yesu akisema kwamba angeteswa, angekufa na kufufuka, na kwamba ingewabidi kumfuata. Kwa siku sita walilitafakari jambo hili!
  • Wazia mwaliko wa kufanya safari hii yenye fumbo ya kupanda mlima, huku yaonekana wakiwa wamejulishwa machache tu mapema kuhusu yale ambayo yangetokea. Jione ukiwa safarini pamoja na hawa watatu.
  • Tafakari wakati Yesu aliposimama na ghafla akageuka sura, aking’aa kwa utukufu. Mtazame Bwana wetu akizungumza na Musa na Eliya. Sikiliza sauti ya Baba iliyo wazi na yenye kunguruma kama radi.
  • Chunguza mawazo na moyo wa Petro. Alisema, “Bwana, ni vizuri sisi kuwa hapa…” Hisia furaha yake, mshangao wake na kicho chake.
  • Keti kwa utulivu ukitafakari tukio hili lote na mazungumzo yao walipokuwa wakishuka mlimani. Unapolitafakari kimya kimya, mngojee Bwana wetu na umruhusu aseme nawe binafsi ikiwa atachagua kufanya hivyo.

Picha Iliyoangaziwa: Kugeuka Sura, na Carl Bloch

Utangulizi wa Tafakari za Kipindi cha Mwaka

  1. Ubatizo wa Bwana
  2. Bendera Mbili
  3. Makundi Matatu ya Watu
  4. Majaribu
  5. Kuitwa kwa Mitume
  6. Arusi ya Kana
  7. Kusafisha Hekalu
  8. Hotuba ya Mlimani
  9. Kuituliza Dhoruba
  10. Kutembea Juu ya Maji
  11. Mitume Walitumwa Kuhubiri
  12. Kuongoka kwa Maria Magdalena
  13. Jinsi Kristo Alivyowalisha Watu Elfu Tano
  14. Kugeuka Sura kwa Kristo
  15. Kufufuka kwa Lazaro
  16. Karamu ya Jioni huko Bethania
  17. Njia Tatu za Unyenyekevu

Yaliyomo

Shiriki ukurasa huu: