Kiswahili

Kufunga na Kujinyima Nyama

Jumatano ya Majivu na Ijumaa Kuu ni siku ambazo Wakatoliki wana wajibu wa kufunga na kujinyima nyama. Aidha, Ijumaa za Kwaresima ni siku ambazo wana wajibu wa kujinyima nyama.

Kwa waamini wa Kanisa Katoliki la Kilatini, kanuni za kufunga ni za lazima kuanzia umri wa miaka 18 hadi miaka 59. Wakati wa kufunga, mtu anaruhusiwa kula mlo mmoja kamili, pamoja na milo miwili midogo ambayo kwa pamoja haifikii mlo mmoja kamili. Kanuni zinazohusu kujinyima nyama zinawafunga waamini wa Kanisa Katoliki la Kilatini kuanzia umri wa miaka 14 na kuendelea

Waamini wa Makanisa Katoliki ya Mashariki wanapaswa kuzingatia sheria maalumu ya Kanisa lao la sui iuris.

Ikiwezekana, mfungo wa Ijumaa Kuu unaendelezwa hadi Mkesha wa Pasaka (usiku wa Jumamosi Kuu) kama “mfungo wa Pasaka” ili kuheshimu mateso na kifo cha Bwana Yesu, na kujiandaa kushiriki kikamilifu zaidi katika Ufufuko Wake na kuusherehekea kwa utayari zaidi.


Chanzo: usccb.org

Shiriki ukurasa huu: