Isaliwe pamoja na watoto wako kabla ya kulala au kabla ya Misa Takatifu ya Jumapili

Bwana wangu Yesu Mtoto, ninakupenda na ninakushukuru kwa kipindi hiki cha Majilio. Tafadhali nisaidie kuelewa yote uliyonitendea. Mama Yako mwenye upendo alikuhifadhi moyoni mwake na kukuleta ulimwenguni humu. Nisaidie kufanya vivyo hivyo.
Yesu wangu mwenye upendo, katika kipindi hiki cha Majilio, ninakuchagua Wewe kuwa Mfalme wangu na Mungu wangu. Nivute karibu Nawe na unisaidie kuziona dhambi zangu ili niweze kubadili mambo unayotaka niyabadili.
Mama Maria, uniombee katika kipindi hiki cha Majilio ili nifanye yote ambayo Mungu anataka nifanye. Ulisema “Ndiyo” kwa yote ambayo Mungu alikuomba. Tafadhali uniombee nami nifanye vivyo hivyo.
Njoo, Bwana Yesu,
Njoo, Bwana Yesu,
Njoo, Bwana Yesu, njoo!
Ninakupenda, Yesu.
Amina.