Kiswahili

Msaada kwa Wenye Sonona

Ee Kristo Yesu,

wakati kila kitu kinapokuwa gizani
nami ninapohisi udhaifu wangu na kutoweza kujisaidia,
nijalie kuhisi uwepo Wako,
upendo Wako, na nguvu Zako.
Nisaidie kuwa na tumaini kamili
katika upendo Wako unaonilinda
na uweza Wako unaonitia nguvu,
ili hakuna kitu kitakachonitisha wala kunitia wasiwasi,
kwa maana, nikiishi karibu Nawe,
nitauona mkono Wako,

kusudi Lako, na mapenzi Yako katika mambo yote.

Amina.

 Na Mtakatifu Inyasi wa Loyola
Shiriki ukurasa huu: