Matukio ya maisha yako huzua maswali
ambayo hayawezi kujibiwa.
Amini kwamba majibu yapo,
lakini huwezi kuyaona.
La muhimu si kuelewa kwako kikamilifu
bali tumaini lako na imani yako tu.
Basi, zingatia kuutumainia wema.
Acha mashaka yako na maswali yako,
kwa kuwa hayakusaidii.
Weka hofu zako kando
na ufungue moyo wako kuzipokea njia Zangu.
Tumaini kwamba wema Wangu upo
katikati ya hali ya kuchanganyikiwa kwa wanadamu.
Tumaini kwamba mkono Wangu unaongoza matukio ya maisha.
Basi, ukiamini hivyo,
kuna haja ya mahangaiko gani?
Basi, ukiwa na imani hii,
unapaswa kubaki na moyo wenye furaha tu.
Mizigo ya maisha haipaswi kukutawala.
Acha mizigo hii
iondoke na kupisha faraja.
Acha maneno Yangu
yauinue moyo wako kwenye furaha na amani.
Acha thawabu hizi
ziujaze moyo wako hali ya kuridhika.
