Kiswahili

KUTOKA UZIMANI HADI MAUTINI

Hali ya kibinadamu niliyoiumba
  ni ili wote waelewe
  maisha mapya yanayowangoja.
Usidhani kwamba hayo ni sawa na yale unayoyapitia
  katika hali yako ya kibinadamu.
Sivyo yalivyo.

Usijaribu kuwazia mapema maisha haya mapya yatakuwaje;
  huwezi kuyaelewa.
Jua tu kwamba yamejaa amani
  na yanazidi yale unayoyaonja na uliyo nayo sasa.
Hayafanani na maisha mengine yoyote.

Utafurahia wakati huu pamoja Nami
  utakapojaliwa wakati huo.
Nitakutunza
  utakapojaliwa kuipitia hali hii.
Litarajie tukio hili kwa furaha
  wala usiogope usiyoyajua.
Ninakupa nyakati zilizojaa amani katika maisha yako ya kibinadamu
  ili uanze kujua
  hazina za kiroho zinazokungojea.

Tafakari Inayofuata

Yaliyomo

Shiriki ukurasa huu: