Kiswahili

Sala ya Krismasi

Heri ya Krismasi!

Utukufu kwa Mungu juu mbinguni!

Bwana wangu mpendwa, Yesu,

Ninakuabudu kwa upendo wa dhati na kufurahia sherehe ya kuzaliwa Kwako.

Upendo Wako kwetu hauna kipimo,

una utukufu

unabadilisha,

unatia kicho,

na unamgusa kila mmoja wetu kwa undani.

Ulichagua kuja na kukaa kati yetu,

ukizaliwa katika umaskini, kukataliwa na unyenyekevu.

Lakini mama Yako alijua ni nani aliyemzaa,

Moyo wake ulijaa upendo wenye huruma nyororo kabisa

alipomwabudu Mtoto wake na Mungu wake.

Nisaidie, Bwana mpendwa.

nifikie kukupenda kwa moyo wa mama Yako.

Nialike nikuabudu pamoja na Mtakatifu Yosefu na wachungaji maskini.

Nifunulie nguvu yenye utukufu ya kuzaliwa Kwako

na ubadilishe maisha yangu kwa sababu ya zawadi hii kamilifu ya Wewe mwenyewe.

Ninakupenda, Bwana Yesu mpendwa.

Nisaidie nikupende kwa moyo wangu wote.

Mwokozi wa Ulimwengu uliyezaliwa sasa,

Nakutumainia.

Mama Maria na Mtakatifu Yosefu,

Niombeeni mimi na watu wote.

Amina.


Tafakari Nyingine za Krismasi:

Shiriki ukurasa huu: