Kiswahili

NIKO PAMOJA NAWE DAIMA

Mashaka yako
  yatakupofusha.
Hofu zako
  zitakuzuia.
Kusitasita kwako
  kutakupotosha.

Yakabidhi matatizo haya
  tena kwa Muumba wake.

Shauku ya asili Yangu
  itakufikisha kwenye asili hiyo.

Kutafuta kwako
  kutakuwezesha kunipata.

Kuwa na subira kwa asili yako
  kutakuwezesha kuelewa asili Yangu.

Utaujua uwepo Wangu
  utakapoifungulia moyo asili Yangu.

Omba unipate,
  nami nitakupata.

Ninyoshee mkono,
  nami nitakuwa hapo pamoja nawe.

Hakuna hata kitambo
  kitakachokupita bila Mimi.
Hakuna tukio hata moja litakaloanza
  na kuisha bila Mimi kuwa nawe.

Tafakari Inayofuata

Yaliyomo

Shiriki ukurasa huu: