Kiswahili

MASHAKA

Yatumainie maneno Yangu yanayokuongoza;
  acha njia zako potovu.
Weka tumaini lako katika njia Yangu
  wala usiwe na shaka kamwe juu ya upendo Wangu.
Sitakupotosha wala kukudhuru.

Basi usiogope
  kile kilichopangwa kwa ajili yako,
  kwa kuwa mkondo wake utakuongoza.
Usikubali kukengeushwa
  na kile kinachoonekana kuwa chenye maumivu.
Bali furahi mizigo ya maisha
  inapokuongoza Kwangu.

Basi, mateso yoyote yanaweza kukuletea baraka
  na kukusaidia kuishi ndani Yangu.

Tafakari Inayofuata

Yaliyomo

Shiriki ukurasa huu: