Umeteseka sana kwa ajili Yangu.
Ni faraja gani basi inaweza kukutia moyo?
Ni maneno gani basi yatakutuliza?
Ni nguvu gani zitakulinda?
Usihangaike kuhusu maswali haya,
kwa maana utapewa yote kadiri utakavyoyahitaji.
Tumainia njia na mbinu Zangu,
kwa maana utalijua kusudi Langu
kadiri mpango Wangu unavyotimia.
Usiache mawazo yako
yajawe na hofu kuhusu makusudi Yangu,
kwa maana kinachohitajika tu ni kuzitumainia njia Zangu.
Hofu yako haiwezi kusaidia kutimiza makusudi Yangu,
kwa maana hofu si sehemu ya mpango Wangu.
Basi yatazame matendo Yangu kwa mtazamo mpya,
kwa maana yatakupa amani na uradhi.
