Kiswahili

HAZINA YANGU

Fungua moyo wako.
Yaachilie mahangaiko yako.
Kwa maana hakuna taabu itakayokumeza,
  unapotembea pamoja Nami.

Na ni majanga gani yanayoweza kukumeza,
  unaponitazamia Mimi?

Hakuna magumu yanayolemea kupita kiasi,
  wala hakuna dhuluma isiyoweza kurekebishwa.

Nitakuokoa katika hali yako ya kutoweza kujisaidia,
  nami nitabadilisha hali yako.
Fuata njia Yangu
  na uruhusu uwepo Wangu ukufariji.

Kwa maana wewe ni hazina Yangu,
  wala hakuna madhara yatakayokulemea.

Tafakari Inayofuata

Yaliyomo

Shiriki ukurasa huu: