
Ee Bwana Yesu, ninakuabudu Wewe, Mwana wa Maria, Mwokozi wangu na Ndugu yangu, kwa kuwa Wewe ni Mungu. Ninakufuata katika mawazo yangu, ee malimbuko ya jamii yetu ya wanadamu, huku nikitumaini siku moja, kwa neema Yako, kukufuata mimi mwenyewe katika utukufu wa mbinguni. Hadi wakati huo, usiniache nipuuze kazi ya hapa duniani uliyonipa. Nijalie nifanye kazi kwa bidii maisha yangu yote, nikiuthamini zaidi wakati wa sasa. Nijalie nitambue kwamba ni kwa kuufikia tu utimilifu wa kweli wa kibinadamu ninaweza kuufikia utimilifu wa Kimungu na kupaa Kwako nitakapomaliza kazi yangu.
Amina.
Masomo ya Ziada – Kupaa Mbinguni
Tafakari kwa ajili ya Kupaa kwa Bwana Mbinguni