Kiswahili

Sala ya Kujikabidhi

Gemäldegalerie Berlin, Milki ya umma, kupitia Wikimedia Commons

Baba,

Ninajikabidhi mikononi Mwako;

unitendee utakavyo.

Lolote utakalonitendea, ninakushukuru:

Niko tayari kwa yote, ninakubali yote.

Yatimizwe ndani yangu mapenzi Yako tu,

na katika viumbe Vyako vyote –

Sitamani zaidi ya hayo, Ee Bwana.

Mikononi Mwako naikabidhi roho yangu:

Ninakutolea kwa upendo wote wa moyo wangu,

kwa maana ninakupenda, Bwana, na hivyo ninahitaji kujitoa,

kujikabidhi mikononi Mwako bila kujibakizia chochote,

na kwa tumaini lisilo na mipaka,

kwa maana Wewe ni Baba yangu.

Amina.

Mtakatifu Charles de Foucauld


Sala Nyingine

Tafakari za Kila Siku

Shiriki ukurasa huu: