Kiswahili

WASIWASI

Kila unapokumbana na maumivu, unaongozwa kugundua mambo mapya.
Yaone mambo haya unayopitia kuwa ya lazima kwa ukuaji wako.

Hakuna maumivu yatakayokulemea.
Hakuna kipindi cha mateso kitakachokuwa cha kupita kiasi.
Mambo haya unayopitia ni sehemu ya hali yako ya kibinadamu.

Ukaribishe wasiwasi huu,
  kwa kuwa utakuongoza kwenye utajiri mpya wa ufahamu.
Usiyaelekezee maumivu fikira zako.
Badala yake,
  karibisha maarifa na uelewa wako mpya,
  kwa kuwa hili ndilo tumaini Langu kwako.

Tazama daima mbele, ng’ambo ya maumivu yako ya sasa,
  uelekee ukuaji mpya ulioandaliwa kwa ajili yako.
Uutazame daima ukuaji huo kama hatua nyingine
  kuelekea kile kinachongoja ukizingatie.
Tafuta mabadiliko yaliyoandaliwa kwa ajili yako.
Furahia matunda yake,
  kwa kuwa manufaa haya ni kwa ajili ya furaha yako.
Ifurahie zawadi hii,
  kwa kuwa imehifadhiwa ili ikuletee raha.

Tafakari Inayofuata

Yaliyomo

Shiriki ukurasa huu: