Uone mkono Wangu uliopo katika maisha yako.
Uruhusu ushawishi Wangu ujulikane
unapoutambua uwepo huu.
Uruhusu uwepo Wangu ukuinue hadi ngazi mpya
ya hekima na utulivu.
Ondoa maishani mwako mambo yanayokuvuruga na kukuzuia
kuutambua kikamilifu uwepo Wangu.
Ni furaha gani kubwa zaidi kuliko hii inayoweza kupatikana?
Ni amani gani kubwa zaidi kuliko hii inayoweza kuonwa?
Uruhusu matunda haya yawe sehemu ya maisha yako.
Uruhusu ufahamu huu uwe ndani yako na uwe wazi kwako.
