Ninasema nawe nyakati za utulivu
ili Neno Langu lijulikane.
Nyakati hizi ni nyakati takatifu
ili upate kunijua zaidi.
Nyakati hizi zinahitajika
ili nikujulishe kinachotakiwa.
Acha nyakati hizi zijazwe neema,
kwa kuwa ni za kukupatia hekima.
Tenga muda wa kuwa nami
ili ulijue Neno Langu,
nami nitazibariki juhudi hizi.
Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi,
wala hofu haipaswi kuwapo,
kwa kuwa MIMI NI Mwokozi wako ninayeleta amani.
