Kiswahili

Sikukuu na Sherehe katika Kipindi cha Kawaida: Majuma 18-34

Utukufu wa Mungu!

Sikukuu ya Kugeuka Sura kwa Bwana, Agosti 6

Yesu aliwachukua Petro, Yakobo, na Yohane ndugu yake, akawapandisha juu ya mlima mrefu faraghani, wakiwa wao tu. Naye akageuka sura mbele yao, na mavazi yake yakawa meupe yenye kung’aa sana, kiasi ambacho hakuna mfuaji duniani angeweza kuyafanya meupe hivyo.ย  Marko 9:2-3

Je, unauona utukufu wa Mungu katika maisha yako? Mara nyingi hili ni jambo gumu kweli. Tunaweza kutambua kwa urahisi matatizo yote tunayokabili na kukazia fikira matatizo hayo. Kwa sababu hiyo, mara nyingi ni rahisi kwetu kushindwa kuuona utukufu wa Mungu katika maisha yetu. Basi, je, unauona utukufu wa Mungu katika maisha yako?

Sikukuu tunayoadhimisha leo ni ukumbusho wa tukio ambalo Yesu aliwafunulia kweli utukufu Wake Mitume watatu. Aliwapandisha kwenye mlima mrefu, akageuka sura mbele yao. Akawa mweupe wa kungโ€™aa na mwenye mngโ€™ao wa utukufu. Hii ilikuwa taswira muhimu kwao kuiweka akilini, ili kujiandaa kwa taswira halisi kabisa ya mateso na kifo ambavyo Yesu alikuwa karibu kuvipitia.

Somo moja tunalopaswa kujifunza kutokana na sikukuu hii ni kwamba utukufu wa Yesu haukupotea Msalabani. Ni kweli kwamba mateso na maumivu Yake yalidhihirika wakati huo, lakini hilo halibadili ukweli kwamba utukufu Wake uliendelea kuwa halisi vilevile hata alipokuwa akiteseka Msalabani.

Ndivyo ilivyo pia katika maisha yetu. Tumebarikiwa kupita kiasi, na Mungu bado anatamani kuzigeuza nafsi zetu ziwe mianga yenye utukufu ya nuru na neema. Anapofanya hivyo, lazima tujitahidi kuutambua daima utendaji huo. Na tunapoteseka au kukabili msalaba fulani, tusigeuze kamwe macho yetu kutoka katika mambo yenye utukufu ambayo ameyatenda ndani ya nafsi zetu.

Tafakari leo juu ya mabadiliko mazuri na ya kina ambayo Mungu ameyafanya na bado anatamani kuyafanya ndani ya nafsi yako. Jua kwamba anataka ukazie macho utukufu huu na uendelee kushukuru daima kwa ajili yake, hasa unapovumilia msalaba wowote uliopewa.

Bwana, nijalie kuuona utukufu Wako na utukufu ambao umeijalia nafsi yangu mwenyewe. Macho yangu yaendelee kuikazia daima neema hiyo. Nijalie kukuona Wewe na utukufu Wako hasa nyakati za shida. Yesu, nakutumainia.


Kutojifungamanisha

Sikukuu ya Mtakatifu Laurenti, Shemasi na Shahidi, Agosti 10

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: โ€œAmina, amina, nawaambieni, chembe ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubaki kuwa chembe moja tu ya ngano; lakini ikifa, huzaa matunda mengi.โ€ย  Yohane 12:24

Hii ni kauli inayovutia, lakini inafunua ukweli ambao ni vigumu kuukubali na kuuishi.ย  Yesu anazungumza moja kwa moja juu ya ulazima wa kujifia mwenyewe ili maisha yako yazae matunda mengi mema.ย  Tena, ni rahisi kusema, lakini ni vigumu kuishi hivyo.

Kwa nini ni vigumu kuishi hivyo?ย  Ugumu wake uko wapi?ย  Ugumu huanza pale tunapopaswa kwanza kukubali ukweli kwamba kujifia mwenyewe ni jambo la lazima na jema.ย  Basi, tuangalie maana yake.

Tunaanza kwa mfano wa punje ya ngano. Punje hiyo lazima ijitenge na suke na kuanguka ardhini. Huu ni mfano wa kujitenga kabisa na vyote tunavyoshikamana navyo. Punje hiyo moja ya ngano lazima โ€œiachilieโ€ kila kitu. Mfano huu unatuambia kwamba ikiwa tunataka Mungu afanye miujiza ndani yetu, lazima tuwe tayari na wenye nia ya kuachilia vyote tunavyoshikamana navyo. Maana yake ni kwamba tunayaachilia kwa dhati mapenzi yetu wenyewe, mapendeleo yetu, matamanio yetu na matumaini yetu. Hili linaweza kuwa gumu sana kulifanya kwa sababu linaweza kuwa gumu sana kulielewa. Inaweza kuwa vigumu kuelewa kwamba kujitenga na yote tunayotaka na kutamani kwa kweli ni jambo jema, na kwa kweli ndiyo njia ya kujiandaa kwa ajili ya maisha mapya na yenye utukufu mkubwa zaidi yanayotungoja kwa njia ya mabadiliko yanayoletwa na neema. Kujifia wenyewe kunamaanisha kumtumainia Mungu zaidi kuliko vitu tunavyoshikamana navyo katika maisha haya. Kunamaanisha kuamini kwamba mpango wa Mungu ni bora kupita kiasi kuliko mpango wowote tunaoweza kubuni.

Punje ya ngano inapokufa na kuingia ardhini, inatimiza kusudi lake na kukua ikizaa mengi zaidi. Inabadilika na kuleta mavuno tele.

Mtakatifu Laurenti, shemasi na mfiadini wa karne ya tatu tunayemkumbuka leo, anatupa mfano halisi wa mtu aliyeacha kila kitu, hata uhai wake mwenyewe, ili kumwambia Mungu โ€œNdiyoโ€. Aliacha utajiri wake wote, na alipoamriwa na mkuu wa Roma akabidhi hazina zote za Kanisa, Laurenti alimletea maskini na wagonjwa. Mkuu huyo, kwa hasira, alimhukumu Laurenti kuuawa kwa moto. Laurenti aliacha kila kitu ili kumfuata Bwana wake.

Tafakari leo kile ambacho huenda Mungu anakuita ukiache. Ni kitu gani anachotaka ukikabidhi Kwake? Kujikabidhi kwa Mungu ndiyo njia ya kumruhusu afanye mambo yenye utukufu katika maisha yako.

Bwana, nisaidie kuacha mapendeleo na mawazo yangu mwenyewe katika maisha ambayo hayapatani na mapenzi Yako ya kimungu. Nisaidie kuamini daima kwamba una mpango ulio bora zaidi pasipo kipimo. Ninapoukubali mpango huo, nisaidie kutumaini kwamba utazaa matunda mengi mema. Yesu, nakutumainia.


Kumpokea Mama wa Mungu kwa Upendo

Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni kwa Bikira Maria Mwenye Heri, Agosti 15

โ€œNafsi yangu inautangaza ukuu wa Bwana; roho yangu inafurahi katika Mungu Mwokozi wangu, kwa maana amemtazama kwa wema mtumishi Wake mnyenyekevu. Tangu siku hii vizazi vyote vitaniita mwenye heri: Mwenyezi amenitendea makuu, na Jina Lake ni takatifu.โ€ Luka 1:46-49

Mistari hii ya mwanzo ya wimbo mtukufu wa sifa wa Mama yetu Mbarikiwa inafunua yeye ni nani. Yeye ndiye ambaye maisha yake yote yanatangaza ukuu wa Mungu na ambaye anashangilia daima. Yeye ndiye kielelezo kamilifu cha unyenyekevu na, kwa hiyo, anayetukuzwa sana na kila kizazi. Yeye ndiye ambaye Mungu amemtendea mambo makuu na ambaye Mungu amemvika utakatifu.

Sherehe tunayoadhimisha leo, ya Kupalizwa kwake Mbinguni, inaonyesha jinsi Mungu anavyoutambua ukuu wake. Mungu hakumruhusu kuonja mauti wala matokeo yoyote ya dhambi. Alikuwa asiye na doa la dhambi, mkamilifu kwa kila namna, tangu alipotungwa mimba hadi alipochukuliwa mbinguni, mwili na roho, ili kutawala akiwa Malkia milele yote.

Hali ya Mama yetu Mwenye Heri ya kutokuwa na doa la dhambi inaweza kuwa vigumu kwa wengine kuielewa. Hiyo ni kwa sababu maisha yake ni mojawapo ya mafumbo makuu zaidi ya imani yetu. Ni machache sana yaliyosemwa juu yake katika Maandiko Matakatifu, lakini mengi yatasemwa juu yake milele yote kadiri unyenyekevu wake unavyofunuliwa na ukuu wake unavyongโ€™aa ili wote wauone.

Mama yetu Mbarikiwa alikuwa Bila Doa, yaani bila dhambi, kwa sababu mbili. Kwanza, Mungu alimkinga dhidi ya dhambi ya asili tangu alipotungwa mimba, kwa neema ya pekee. Tunaiita hii โ€œneema ya kukinga.โ€ Kama Adamu na Eva, alitungwa mimba bila dhambi. Lakini tofauti na Adamu na Eva, yeye alitungwa mimba katika hali ya neema. Alitungwa mimba akiwa tayari ameokolewa kwa neema, na Mwanawe ambaye siku moja angemleta ulimwenguni. Neema ambayo Mwanawe angeimimina siku moja juu ya ulimwengu ilivuka mipaka ya wakati na kumfunika tangu alipotungwa mimba.

Sababu ya pili ya Mama yetu Mwenye Heri kutokuwa na doa la dhambi ni kwamba, tofauti na Adamu na Eva, hakuchagua kamwe kutenda dhambi katika maisha yake yote. Kwa hiyo, akawa Eva mpya, Mama mpya wa wote Walio Hai, Mama mpya wa wote wanaoishi katika neema ya Mwana wake. Kwa sababu ya hali hii ya kutokuwa na doa la dhambi na uchaguzi wake wa hiari wa kuendelea kuishi katika neema, Mungu alimchukua mbinguni, mwili na roho, alipomaliza maisha yake ya duniani. Ni tukio hili lenye utukufu na adhama tunaloliadhimisha leo.

Tafakari leo jinsi unavyomwelewa Mama yetu Mwenye Heri. Je, unamjua, unaelewa nafasi yake katika maisha yako, na daima unatafuta malezi yake ya kimama? Yeye ni mama yako ikiwa unachagua kuishi katika neema ya Mwana wake. Ikubali kweli hiyo kwa undani zaidi leo na uchague kumpa nafasi muhimu zaidi katika maisha yako. Yesu atakushukuru kwa kufanya hivyo!

Bwana, nisaidie kumpenda mama Yako kwa upendo uleule ulio nao kwake. Kama Wewe ulivyokabidhiwa kwenye uangalizi wake, nami natamani kukabidhiwa kwenye uangalizi wake. Maria, Mama yangu na Malkia wangu, uniombee ninapokukimbilia. Yesu, nakutumainia.


Mama Yetu Mbarikiwa: Malkia wa Watakatifu Wote!

Kumbukumbu ya Umalkia wa Bikira Maria Mbarikiwa, Agosti 22

Kifungu kifuatacho kimetolewa katika Imani Yangu Katoliki!, Sura ya 8:

Njia bora zaidi ya kuhitimisha kitabu hiki ni kutafakari jukumu la mwisho na lenye utukufu la Mama yetu Mbarikiwa akiwa Malkia na Mama wa watakatifu wote katika enzi hii mpya inayokuja. Tayari alitimiza jukumu muhimu katika wokovu wa ulimwengu, lakini kazi yake bado haijaisha. Kwa Kutungwa kwake Mimba Bila Dhambi ya Asili, akawa chombo kikamilifu cha Mwokozi na, kwa hiyo, Mama mpya wa wote walio hai. Akiwa mama huyu mpya, anabatilisha kutotii kwa Eva kwa kuendelea kuchagua kwa uhuru kushirikiana kikamilifu na mpango wa Mungu na kuutii. Msalabani, Yesu alimkabidhi mama Yake kwa Yohane, jambo ambalo ni ishara ya kwamba alitukabidhi sisi sote mama huyo awe mama yetu mpya. Kwa hiyo, kwa kadiri tulivyo viungo vya Mwili wa Kristo, viungo vya Mwili wa Mwana wake, sisi pia, kama mpango wa Mungu unavyohitaji, ni watoto wa mama huyu mmoja.

Mojawapo ya mafundisho ya imani yetu yaliyotangazwa rasmi kuwa kweli za imani ni kwamba, alipomaliza maisha yake hapa duniani, Mama Yetu Mbarikiwa alipalizwa Mbinguni kwa mwili na roho ili awe pamoja na Mwanawe milele yote.ย  Na sasa, akiwa mahali pake Mbinguni, amepewa cheo cha pekee kabisa cha Malkia wa Wote Walio Hai!ย  Yeye ni Malkia wa Ufalme wa Mungu sasa, na atakuwa Malkia wa Ufalme huu milele yote!

Akiwa Malkia, pia anafurahia zawadi ya pekee kabisa ya kuwa mpatanishi na mgawaji wa neema.ย  Jambo hili linaeleweka vizuri zaidi kwa namna hii:

  • Alikingwa dhidi ya dhambi zote tangu alipotungwa mimba bila doa la dhambi ya asili;
  • Kwa hiyo, alikuwa chombo pekee cha kibinadamu kilichofaa ambacho kwa njia yake Mungu angeweza kutwaa mwili;
  • Mungu Mwana alitwaa mwili kweli kwa njia yake, kwa uwezo na utendaji wa Roho Mtakatifu;
  • Kwa njia ya Mwana huyu mmoja wa kimungu, sasa akiwa katika mwili, wokovu wa ulimwengu ulipatikana;
  • Zawadi hii ya wokovu inatufikia kwa njia ya neema. Neema huja hasa kwa njia ya sala na sakramenti;
  • KWA HIYO, kwa kuwa Maria alikuwa chombo ambacho kwa njia yake Mungu aliingia katika ulimwengu wetu, yeye pia ni chombo ambacho kwa njia yake neema YOTE huja. Yeye ni chombo cha yote yaliyotokana na Umwilisho. Kwa hiyo, yeye ni Mpatanishi wa Neema!

Kwa maneno mengine, tendo la Maria la upatanishi katika Umwilisho halikuwa tu tendo fulani la kihistoria lililotokea zamani sana. Badala yake, umama wake ni jambo linaloendelea na la milele. Ni umama wa daima kwa Mwokozi wa ulimwengu, naye ni chombo cha daima ambacho kwa njia yake tunapokea yote yanayotujia kutoka kwa Mwokozi huyu.

Mungu ndiye chanzo, lakini Maria ndiye chombo.ย  Naye ni chombo kwa sababu Mungu alitaka iwe hivyo.ย  Hawezi kufanya chochote kwa uwezo wake mwenyewe, lakini wala hahitaji kufanya hivyo kwa uwezo wake mwenyewe.ย  Yeye si Mwokozi.ย  Yeye ni chombo.

Kwa sababu hiyo, lazima tuione nafasi yake kuwa yenye utukufu na ya lazima katika mpango wa milele wa wokovu. Ibada ya heshima kwake ni njia ya kukiri tu kilicho kweli. Si heshima fulani tu tunayompa kwa kumshukuru kwa kushirikiana na mpango wa Mungu. Badala yake, ni kukiri nafasi yake inayoendelea ya upatanishi wa neema katika ulimwengu wetu na katika maisha yetu.

Akiwa Mbinguni, Mungu hamnyang’anyi jukumu hili. Badala yake, anafanywa kuwa Mama yetu na Malkia wetu. Naye kwa kweli ni Mama na Malkia anayestahili!

Salamu, Malkia Mtakatifu, Mama wa Huruma, uzima wetu, utamu wetu na tumaini letu! Tunakulilia wewe, sisi wana maskini wa Eva waliohamishwa. Tunakuletea miguno yetu, tukiomboleza na kulia katika bonde hili la machozi! Basi, ewe Mwombezi mwenye fadhili nyingi, utugeuzie macho yako yenye huruma, na baada ya uhamisho wetu huu, utuonyeshe Yesu, mzao mbarikiwa wa tumbo lako. Ewe mwenye huruma, ewe mwenye upendo, ewe Bikira Maria mtamu.

V. Utuombee, ee Mama Mtakatifu wa Mungu.
R. Ili tustahili ahadi za Kristo.


Bila Unafiki wala Hila

Sikukuu ya Mtakatifu Bartolomayo, Mtume, Agosti 24

Yesu alimwona Natanaeli akija Kwake, akasema juu yake, โ€œHuyu hapa ni mwana wa kweli wa Israeli. Hana unafiki ndani yake.โ€ Natanaeli akamwambia, โ€œUnanijuaje?โ€ Yesu akamjibu, โ€œKabla Filipo hajakuita, nilikuona chini ya mtini.โ€ Natanaeli akamjibu, โ€œRabi, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu; Wewe ndiwe Mfalme wa Israeli.โ€ Yohane 1:47-49

Unaposoma kifungu hiki kwa mara ya kwanza, huenda ukahisi haja ya kurudi na kukisoma tena. Ni rahisi kukisoma na kufikiri kwamba kuna jambo fulani ambalo hukuliona. Inakuwaje kwamba Yesu alimwambia tu Natanaeli (anayeitwa pia Bartolomayo) kwamba alimwona ameketi chini ya mtini, na hilo likatosha kumfanya Natanaeli ajibu, โ€œRabi, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu; Wewe ndiwe Mfalme wa Israeli.โ€ Ni rahisi kushangaa jinsi Natanaeli alivyoweza kufikia hitimisho hilo kutokana na maneno ambayo Yesu alisema juu yake.

Lakini angalia jinsi Yesu alivyomwelezea Natanaeli. Alikuwa mtu โ€œasiye na unafiki.โ€ Tafsiri nyingine zinasema alikuwa โ€œhana hila.โ€ Basi, maana yake ni nini?

Mtu akiwa na unafiki au hila, maana yake ni kwamba ana nyuso mbili na ni mjanja wa kudanganya. Ana ustadi wa kuwadanganya wengine. Hii ni tabia hatari na yenye kuleta maangamizi. Lakini kusema kinyume chake, kwamba mtu โ€œhana unafikiโ€ au โ€œhana hila,โ€ ni njia ya kusema kwamba yeye ni mwaminifu, mnyofu, mkweli, wazi na asiyejifanya.

Kwa upande wa Natanaeli, alikuwa mtu aliyesema kwa uhuru yale aliyowaza. Katika tukio hili, haikuwa kwamba Yesu alitoa hoja fulani ya kiakili yenye kusadikisha kuhusu umungu Wake; hakusema chochote kuuhusu. Badala yake, kilichotokea ni kwamba fadhila hii njema ya Natanaeli, ya kutokuwa na unafiki, ilimwezesha kumtazama Yesu na kutambua kwamba Yeye ndiye โ€œwa kweli kabisa.โ€ Mazoea mema ya Natanaeli ya kuwa mwaminifu, mkweli na muwazi yalimwezesha si tu kudhihirisha Yesu ni nani, bali pia kuwaona wengine kwa uwazi na ukweli zaidi. Na sifa hii ilimsaidia sana alipomwona Yesu kwa mara ya kwanza na kuweza kutambua mara moja ukuu wa Yeye alivyo.

Tafakari leo ni kwa kiasi gani uko huru kutoka katika hila na unafiki. Je, wewe pia ni mtu mwenye uaminifu mkubwa, ukweli na uwazi? Je, kweli uko jinsi unavyoonekana kuwa? Kuishi namna hii ndiyo njia pekee nzuri ya kuishi. Ni maisha yanayoishiwa katika ukweli. Sali ili Mungu akusaidie kukua katika fadhila hii leo kwa maombezi ya Mtakatifu Bartolomayo.

Bwana, nisaidie kuwa huru na unafiki na hila.ย  Nisaidie kuwa mtu mwaminifu, mwadilifu na mnyofu wa moyo.ย  Asante kwa mfano uliowekwa na Mtakatifu Bartholomayo.ย  Nipe neema ninayohitaji ili kuiga fadhila zake.ย  Yesu, nakutumainia.


Uaminifu Katika Mateso

Kumbukumbu ya Mateso ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji, Agosti 29

Msichana yule aliharakisha kurudi mbele ya mfalme na kutoa ombi lake, โ€œNataka unipe sasa hivi kichwa cha Yohane Mbatizaji kwenye sinia.โ€ย  Mfalme alihuzunika sana, lakini kwa sababu ya viapo vyake na wageni hakutaka kuvunja ahadi aliyompa. Kwa hiyo mara moja akamtuma mwuaji akiwa na amri ya kuleta kichwa chake.ย  Marko 6:25-27

Simulizi hili la kusikitisha la kukatwa kichwa kwa Yohane Mbatizaji linatufunulia mambo mengi. Zaidi ya yote, linatufunulia fumbo la uovu katika ulimwengu wetu na mapenzi ya Mungu yanayoruhusu uovu, nyakati fulani, kustawi.

Kwa nini Mungu aliruhusu Mtakatifu Yohane akatwe kichwa? Alikuwa mtu mkuu. Yesu Mwenyewe alisema kwamba hakuna aliyezaliwa na mwanamke aliye mkuu kuliko Yohane Mbatizaji. Hata hivyo, alimruhusu Yohane ateseke kwa kudhulumiwa kiasi hicho.

Mtakatifu Teresa wa Avila alimwambia Bwana wetu wakati mmoja, โ€œBwana mpendwa, ikiwa hivi ndivyo unavyowatendea rafiki Zako, si ajabu kwamba una rafiki wachache sana!โ€ Ndiyo, ni wazi kwamba katika historia yote Mungu ameruhusu wale anaowapenda wateseke sana. Hili linatuambia nini?

Kwanza kabisa, tusisahau ukweli ulio wazi kwamba Baba alimruhusu Mwana ateseke sana na kuuawa kwa namna ya kutisha. Kifo cha Yesu kilikuwa cha kikatili na cha kushtua. Je, hii ina maana kwamba Baba hakumpenda Mwana? La hasha. Basi hii ina maana gani?

Ukweli ni kwamba mateso si ishara ya kutopata kibali mbele ya Mungu.ย  Ukiteseka na Mungu asikupatie nafuu, si kwa sababu Mungu amekuacha.ย  Si kwamba hakupendi.ย  Kwa kweli, kuna uwezekano mkubwa kwamba hali ni kinyume kabisa.

Kwa kweli, mateso ya Yohane Mbatizaji ndiyo mahubiri makuu zaidi ambayo angeweza kuhubiri. Ni ushuhuda wa upendo wake thabiti kwa Mungu na wa kujitoa kwake kwa moyo wote kutimiza mapenzi ya Mungu. โ€œMahubiriโ€ ya mateso ya Yohane yana nguvu kwa sababu alichagua kubaki mwaminifu kwa Bwana wetu licha ya dhuluma alizovumilia. Na mbele ya Mungu, uaminifu wa Yohane una thamani kubwa isiyo na kipimo kuliko kuendelea kwake kuishi katika mwili au mateso ya kimwili aliyovumilia.

Tafakari leo kuhusu maisha yako mwenyewe. Nyakati fulani tunabeba msalaba mzito na kumsihi Bwana wetu atuondolee. Badala yake, Mungu anatuambia kwamba neema Yake inatosha na kwamba anataka kutumia mateso yetu kama ushuhuda wa uaminifu wetu. Kwa hiyo, jibu la Baba kwa Yesu, jibu Lake kwa Yohane na jibu Lake kwetu ni mwito wa kuingia katika fumbo la mateso yetu katika maisha haya tukiwa na imani, matumaini, tumaini thabiti na uaminifu. Kamwe usiruhusu magumu ya maisha yakuzuie kuwa mwaminifu kwa mapenzi ya Mungu.

Bwana, nijalie kuwa na nguvu za Mwana Wako na nguvu za Mtakatifu Yohane Mbatizaji ninapobeba misalaba yangu mwenyewe maishani.ย  Nibaki imara katika imani na kujaa matumaini ninapokusikia ukiniita kuukumbatia msalaba wangu.ย  Yesu, nakutumainia.


Heri ya Siku ya Kuzaliwa, Mama Mbarikiwa!

Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bikira Maria Mbarikiwa, Septemba 8

โ€œTazama, bikira atachukua mimba na kuzaa mwana, nao watamwita jina lake Emanueli.โ€ Mathayo 1:23

Sote tunapenda kusherehekea siku za kuzaliwa. Leo ni sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa mama yetu mpendwa. Mwezi Desemba tunamheshimu kwa kukingwa kwake dhambi ya asili tangu kutungwa mimba. Mwezi Januari tunamsherehekea kama Mama wa Mungu. Mwezi Agosti tunasherehekea Kupalizwa kwake Mbinguni, na kuna siku nyingine nyingi katika mwaka tunapoheshimu kipengele cha pekee cha maisha yake. Lakini leo ni sherehe tu ya siku yake ya kuzaliwa!

Kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ni namna ya kuadhimisha utu wake.ย  Tunamsherehekea kwa sababu tu yeye ni yeye.ย  Leo si lazima tuzingatie mojawapo ya mambo ya kipekee, mazuri na ya kina katika maisha yake.ย  Si lazima tutazame yote aliyotimiza, kukubali kwake kikamilifu mapenzi ya Mungu, kuvikwa kwake taji Mbinguni, kupalizwa kwake Mbinguni au mambo mengine yoyote mahususi.ย  Mambo yote ya maisha yake yana utukufu, ni mazuri, yanaamsha kicho na yanastahili kuwa na sikukuu na maadhimisho yake ya pekee.

Hata hivyo, leo tunamsherehekea tu Mama yetu Mbarikiwa kwa sababu aliumbwa na kuletwa ulimwenguni na Mungu, na hilo pekee linastahili kuadhimishwa.ย  Tunamheshimu kwa sababu tu tunampenda, na tunaadhimisha siku yake ya kuzaliwa kama vile tungeadhimisha siku ya kuzaliwa ya mtu yeyote tunayempenda na kumjali.

Tafakari leo ukweli kwamba Mama Maria ni mama yako.ย  Yeye kweli ni mama yako, na inafaa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa namna ileile ambayo ungeadhimisha siku ya kuzaliwa ya mtu yeyote wa familia yako.ย  Kumheshimu Maria leo ni namna ya kuimarisha uhusiano wako naye na kumhakikishia kwamba unatamani awe sehemu muhimu ya maisha yako.

Heri ya siku ya kuzaliwa, Mama Mbarikiwa! Tunakupenda sana!

Salamu Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe.ย  Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa.ย  Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu.ย  Amina.ย  Yesu mpendwa, kwa njia ya moyo wa Bikira Maria asiye na doa, Mama yetu, tunakutumainia!


Msalaba Mtukufu wa Bwana Wetu!

Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu, Septemba 14

โ€œNa kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Mtu lazima ainuliwe, ili kila anayemwamini awe na uzima wa milele.โ€ Yohane 3:14-15

Ni sikukuu tukufu iliyoje tunayoadhimisha leo!ย  Ni Sikukuu ya Kutukuka kwa Msalaba Mtakatifu!

Je, Msalaba una maana kweli?ย  Kama tungeweza kujiweka kando na yote tuliyojifunza kuhusu Msalaba wa Kristo na kuutazama tu kwa mtazamo wa kidunia na wa kihistoria, Msalaba ni ishara ya msiba mkubwa.ย  Unahusiana na habari ya mtu aliyependwa sana na wengi, lakini aliyechukiwa vikali na wengine.ย  Hatimaye, wale waliomchukia mtu huyu walipanga asulubiwe kikatili.ย  Kwa hiyo, kwa mtazamo wa kidunia pekee, Msalaba ni jambo la kutisha.

Lakini Wakristo hawautazami Msalaba kwa mtazamo wa kidunia.ย  Tunautazama kwa mtazamo wa Mungu.ย  Tunamwona Yesu ameinuliwa Msalabani ili wote wamwone.ย  Tunamwona akitumia mateso ya kutisha kuondoa mateso milele.ย  Tunamwona akitumia kifo kuangamiza kifo chenyewe.ย  Hatimaye, tunamwona Yesu akishinda juu ya Msalaba huo na, kwa hiyo, tunauona Msalaba milele kuwa kiti cha enzi kilichotukuzwa na chenye utukufu!

Matendo ya Musa jangwani yalikuwa mfano uliotangulia kuashiria Msalaba.ย  Watu wengi walikuwa wakifa kutokana na kuumwa na nyoka. Kwa hiyo, Mungu alimwambia Musa ainue sanamu ya nyoka juu ya mti ili wote watakaoitazama waponywe.ย  Na ndivyo ilivyotokea hasa.ย  Kwa namna ya kushangaza, nyoka alileta uzima badala ya kifo!

Tunapatwa na mateso kwa namna mbalimbali katika maisha yetu yote.ย  Labda kwa wengine ni maumivu ya kila siku yanayotokana na afya dhaifu, na kwa wengine yanaweza kuwa ya ndani zaidi, kama vile mateso ya kihisia, ya kibinafsi, ya mahusiano au ya kiroho.ย  Kwa kweli, dhambi ndiyo chanzo cha mateso makubwa zaidi, hivyo wale wanaopambana sana na dhambi katika maisha yao huteseka sana kutokana na dhambi hiyo.

Basi, jibu la Yesu ni nini?ย  Jibu Lake ni tuelekeze macho yetu kwenye Msalaba Wake.ย  Tunapaswa kumtazama katika uchungu na mateso Yake na, tunapomtazama hivyo, tunaitwa kuona ushindi kwa imani.ย  Tunaitwa kujua kwamba Mungu huleta mema kutokana na mambo yote, hata mateso yetu.ย  Baba aliubadilisha ulimwengu milele kwa njia ya mateso na kifo cha Mwana Wake wa pekee.ย  Anataka pia kutubadilisha katika misalaba yetu.

Tafakari leo juu ya Msalaba wa Kristo.ย  Tumia muda fulani kuutazama msalaba wenye sura ya Yesu aliyesulubiwa.ย  Katika msalaba huo, ona jibu la mahangaiko yako ya kila siku.ย  Yesu yuko karibu na wale wanaoteseka, na nguvu Zake zinapatikana kwa wote wanaomwamini.

Bwana, nisaidie kuutazama Msalaba.ย  Nisaidie kuonja ushindi Wako wa mwisho ndani ya mateso Yako mwenyewe.ย  Niimarishwe na kuponywa ninapokutazama.ย  Yesu, nakutumainia.


Moyo Wenye Machungu wa Mama Yetu Mbarikiwa

Kumbukumbu ya Bibi Yetu wa Machungu, Septemba 15

โ€œTazama, mtoto huyu amewekwa kwa ajili ya kuanguka na kuinuka kwa wengi katika Israeli, na kuwa ishara itakayopingwa; nawe mwenyewe upanga utakuchoma, ili mawazo ya mioyo mingi yafunuliwe.โ€ย  Luka 2:34-35

Ni sikukuu yenye kina, maana na uhalisi mkubwa tunayoisherehekea leo.ย  Leo tunajaribu kuingia katika machungu makubwa ya moyo wa Mama yetu Mbarikiwa alipostahimili mateso ya Mwanawe.

Mama Maria alimpenda Mwanawe Yesu kwa upendo mkamilifu wa mama.ย  Jambo la kuvutia ni kwamba upendo huo mkamilifu aliokuwa nao moyoni mwake kwa Yesu ndio uliokuwa chanzo cha mateso yake makubwa ya kiroho.ย  Upendo wake ulimvuta kuwa karibu na Yesu katika Msalaba na mateso Yake.ย  Na kwa sababu hiyo, Yesu alipoteseka, mama Yake naye aliteseka.

Lakini mateso yake hayakuwa ya kukata tamaa, yalikuwa mateso ya upendo.ย  Kwa hiyo, uchungu wake haukuwa huzuni tu; bali ulikuwa ushiriki wa kina katika yote ambayo Yesu alivumilia.ย  Moyo wake ulikuwa umeungana kikamilifu na moyo wa Mwanawe na, kwa hiyo, alivumilia yote ambayo Yeye alivumilia.ย  Huu ni upendo wa kweli katika kina chake kikubwa zaidi na uzuri wake mkuu zaidi.

Leo, katika adhimisho hili la kumbukumbu ya Moyo wake Wenye Uchungu, tunaitwa kuishi kwa kuungana na uchungu wa Mama Mbarikiwa.ย  Tunapompenda, tunajikuta tukihisi maumivu na mateso yaleyale ambayo moyo wake bado unayapata kutokana na dhambi za ulimwengu.ย  Dhambi hizo, zikiwemo dhambi zetu wenyewe, ndizo zilizompigilia Mwanawe misumari Msalabani.

Tunapompenda Mama yetu Mbarikiwa na Mwanawe Yesu, sisi pia tutahuzunika kwa sababu ya dhambi; kwanza dhambi zetu wenyewe, kisha dhambi za wengine.ย  Lakini ni muhimu kujua kwamba machungu tunayopata kwa sababu ya dhambi pia ni machungu ya upendo.ย  Ni machungu matakatifu ambayo hatimaye yanatuchochea kuwa na huruma ya kina zaidi na umoja wa ndani zaidi na wale wanaotuzunguka, hasa waliojeruhiwa na walionaswa katika dhambi.ย  Pia yanatuchochea kuziacha dhambi katika maisha yetu wenyewe.

Tafakari leo juu ya upendo mkamilifu wa moyo wa Mama yetu Mbarikiwa.ย  Upendo huo unaweza kuyashinda mateso na maumivu yote, nao ndio upendo ambao Mungu anataka kuuweka moyoni mwako.

Bwana, nisaidie kupenda kwa upendo wa Mama Yako mpendwa.ย  Nisaidie kuhisi uchungu uleule mtakatifu aliouhisi na kuuruhusu uchungu huo mtakatifu kuongeza jinsi ninavyowajali na kuwahurumia wote wanaoteseka. Mama Maria, utuombee.ย Yesu, nakutumainia.


Kuitikia Wito

Sikukuu ya Mtakatifu Mathayo, Mtume na Mwinjili, Septemba 21

Yesu alipokuwa akipita kutoka hapo, alimwona mtu aitwaye Mathayo ameketi kwenye kituo cha ushuru. Akamwambia, โ€œNifuate.โ€ Naye akainuka, akamfuata.ย  Mathayo 9:9

Mtakatifu Mathayo alikuwa mtu tajiri na โ€œmuhimuโ€ katika enzi zake.ย  Akiwa mtoza ushuru, pia hakupendwa na Wayahudi wengi.ย  Lakini alijionyesha kuwa mtu mwema kwa kuitikia mara moja wito wa Yesu.

Hatuna maelezo mengi kuhusu simulizi hili, lakini tuna maelezo yaliyo muhimu. Tunaona kwamba Mathayo yuko kazini akikusanya ushuru. Tunaona kwamba Yesu anapita tu karibu naye na kumwita. Na tunaona kwamba Mathayo anainuka mara moja, anaacha kila kitu, na kumfuata Yesu. Hakika huku ni kuongoka kwa namna ya pekee.

Kwa watu wengi, kuitikia mara moja namna hii kusingetokea. Watu wengi wangehitaji kwanza kumfahamu Yesu, kushawishiwa naye, kuzungumza na familia na marafiki zao, kufikiri, kutafakari, na kisha kuamua ikiwa kumfuata Yesu ni jambo jema. Watu wengi hutumia muda mrefu kuyapima mapenzi ya Mungu kwa akili zao kabla ya kuyaitikia. Je, wewe uko hivyo?

Kila siku Mungu anatuita. Kila siku anatuita tumtumikie kwa kujitoa bila kubakiza chochote na kikamilifu kwa namna moja au nyingine. Na kila siku tuna nafasi ya kuitikia kama Mathayo alivyofanya. Jambo la msingi ni kuwa na sifa mbili muhimu. Kwanza, ni lazima tuitambue sauti ya Yesu kwa uwazi na bila kuikosea. Kwa imani, ni lazima tujue anachotuambia wakati anapotuambia. Pili, ni lazima tuwe na hakika kwamba chochote ambacho Yesu anatuita au kutuvuvia tukifanye kinastahili kufanywa. Tukiweza kuzikamilisha sifa hizi mbili, tutaweza kuiga mwitikio wa haraka na wa kujitoa kabisa wa Mtakatifu Mathayo.

Tafakari leo juu ya utayari wako wa kumwiga Mtume huyu. Unasema na kufanya nini Mungu anapokuita kila siku? Pale unapoona upungufu, jitoe upya kumfuata Kristo bila kubakiza chochote. Hutajuta.

Bwana, nijalie nikusikie ukisema nami na nikuitikie kwa moyo wangu wote kila wakati.ย  Nikufuate popote unaponiongoza.ย  Yesu, nakutumainia.


Malaika Wakuu

Sikukuu ya Watakatifu Mikaeli, Gabrieli na Rafaeli, Malaika Wakuu, Septemba 29

โ€œAmina, amina, nawaambieni, mtaona mbingu imefunguka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Mtu.โ€ Yohane 1:51

Ndiyo, malaika wapo kweli. Nao wana nguvu, utukufu, uzuri na fahari kwa kila namna. Leo tunawaheshimu watatu kati ya umati wa malaika walioko Mbinguni: Mikaeli, Gabrieli na Rafaeli.

Malaika hawa ni โ€œmalaika wakuu.โ€ย  Malaika wakuu ni daraja la pili la malaika, lililo juu kidogo ya malaika walinzi.ย  Kwa jumla, kuna madaraja tisa ya viumbe wa mbinguni ambao kwa kawaida tunawaita malaika, na kwa mapokeo madaraja haya yote tisa yamegawanywa katika makundi matatu.ย  Kwa mapokeo, mpangilio mzima wa madaraja hayo uko hivi:

Kundi la Juu Kabisa: Maserafi, Makerubi na Viti vya Enzi.

Kundi la Kati: Utawala, Nguvu na Mamlaka.

Kundi la Chini: Wakuu, Malaika Wakuu na Malaika (Malaika Walinzi).

Madaraja ya viumbe hawa wa mbinguni yamepangwa kulingana na kazi na madhumuni yao. Viumbe wa daraja la juu kabisa, Maserafi, waliumbwa kwa kusudi moja tu: kukizunguka Kiti cha Enzi cha Mungu wakimwabudu daima. Viumbe wa daraja la chini kabisa, Malaika Walinzi, waliumbwa kwa kusudi la kuwatunza wanadamu na kuwasilisha ujumbe wa Mungu. Malaika Wakuu, ambao tunawaheshimu leo, waliumbwa kwa kusudi la kutuletea ujumbe wenye umuhimu mkubwa na kutekeleza kazi zenye umuhimu mkubwa kabisa katika maisha yetu.

Mikaeli anajulikana sana kuwa malaika mkuu aliyepewa uwezo na Mungu wa kumfukuza Lusifa kutoka Mbinguni. Kwa mapokeo, Lusifa hufikiriwa kuwa wa kundi la juu kabisa la viumbe wa mbinguni; kwa hiyo, kufukuzwa na malaika mkuu wa daraja la chini kulikuwa fedheha kubwa sana kwake.

Gabrieli anajulikana sana kuwa malaika mkuu aliyemletea Bikira Maria Mbarikiwa ujumbe wa Umwilisho.

Naye Rafaeli, ambaye jina lake linamaanisha โ€œMungu anaponya,โ€ anatajwa katika Kitabu cha Tobiti cha Agano la Kale, na inasemekana kwamba alitumwa kuyaponya macho ya Tobiti.

Ingawa hakuna mengi yanayojulikana kuhusu malaika hawa wakuu, ni muhimu kuamini kuwa wapo, kuwaheshimu na kusali kwao. Tunasali kwao kwa sababu tunaamini kwamba Mungu amewakabidhi utume wa kutusaidia kuleta uponyaji, kupambana na uovu na kulitangaza Neno la Mungu. Nguvu zao zinatoka kwa Mungu, lakini Mungu amechagua kuwatumia malaika wakuu, pamoja na viumbe wote wa mbinguni, kutimiza mpango na kusudi Lake.

Tafakari leo juu ya ufahamu wako kuhusu malaika. Je, unaamini kuwa wapo? Je, unawaheshimu? Je, unategemea maombezi na upatanishi wao wenye nguvu katika maisha yako? Mungu anataka kuwatumia, kwa hiyo unapaswa kweli kutafuta msaada wao katika maisha yako.

Bwana, asante kwa zawadi ya Malaika Wakuu tunaowaheshimu leo.ย  Asante kwa kazi yao yenye nguvu katika maisha yetu.ย  Utusaidie kuwategemea na kuwapenda kwa ajili ya huduma yao.ย  Malaika Wakuu, mtuombee, mtuponye, mtufundishe na mtulinde.ย  Yesu, nakutumainia.


Ua Dogo

Kumbukumbu ya Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu wa Lisieux, Oktoba 1

Leo Kanisa letu linamheshimu Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu wa Lisieux. Teresia alifariki mwaka 1897 akiwa na umri mdogo wa miaka ishirini na minne. Alitangazwa kuwa mtakatifu miaka ishirini na minane tu baadaye, mwaka 1925. Mwaka 1997, miaka mia moja baada ya kifo chake, Papa Yohane Paulo II alimtangaza kuwa Mwalimu wa Kanisa. Alihisi kuitwa kuingia katika maisha ya kitawa ya ndani akiwa na umri mdogo, na alijiunga na Wakarmeli akiwa na umri wa miaka kumi na mitano. Miaka yake tisa ndani ya monasteri hiyo ilizaa matunda mema mengi kwa Kanisa zima.

Simulizi moja katika tawasifu ya Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu inaeleza jinsi alivyogundua wito wake. Wakati alipokuwa Karmeli, alikuwa na hamu takatifu ya kumtumikia Kristo kwa njia nyingi. Nyakati fulani alitamani kuwa mmisionari, kwenda kuhubiri Injili na kuleta mabadiliko ya kweli ulimwenguni kwa ajili ya Kristo. Siku moja, alipokuwa akitafakari mwito na wito wake mwenyewe, alitambua kwamba utume wake ulikuwa kuwa moyo wa Kristo. Wengine wameitwa kuwa mikono na miguu Yake, wengine kuwa kinywa Chake, lakini yeye aliitwa kuwa moyo Wake, aliitwa kuwa upendo. Na alipogundua wito wake wa kuwa upendo, alitambua kwamba aliitwa kuwa kila kitu, kwa kuwa upendo ndio wito mkuu kuliko yote.

Yesu anahitaji wafanyakazi kwa ajili ya shamba Lake la mizabibu. Anahitaji sisi sote tujitoe kufanya mapenzi Yake. Zaidi ya yote, anahitaji watu waliojitoa kumwiga Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu kwa kuwa moyo Wake katika ulimwengu usio na upendo. Anahitaji ushuhuda wa mapendo ya kina na ya dhati kuliko kitu kingine chochote.

Tafakari leo juu ya wito wako mwenyewe wa kuwa moyo wa Kristo. Je, unajiona kuwa mtu anayeleta upendo Wake ulimwenguni? Je, umeuitikia kwa kusema โ€œNdiyoโ€ wito huu mtakatifu wa mapendo? Uwe moyo Wake, nawe utaona jinsi anavyowabadilisha wengine kwa upendo unaodhihirishwa kupitia Moyo huo Mtakatifu.

Bwana, ninatamani kweli kuupeleka upendo Wako ulimwenguni. Ninatamani kuwa moyo Wako na hivyo kuwa kila kitu. Angaza ndani yangu na unisaidie kuwa chombo cha huruma Yako kamilifu. Yesu, nakutumainia.


Malaika Walinzi

Kumbukumbu ya Malaika Watakatifu Walinzi, Oktoba 2

โ€œAngalieni msimdharau hata mmoja wa wadogo hawa, kwa maana nawaambia kwamba malaika wao mbinguni daima wanautazama uso wa Baba yangu wa mbinguni.โ€ Mathayo 18:10

Leo tunawaheshimu Malaika Walinzi wetu wenye utukufu! Wao ni hazina na wasaidizi kuliko tunavyoweza kufikiria.

Siku chache zilizopita tuliwaheshimu Malaika Wakuu, Mikaeli, Gabrieli na Rafaeli. Katika tafakari hiyo tulitazama madaraja ya viumbe wa mbinguni walioumbwa na Mungu. Ingawa Malaika Walinzi wako mwisho wa orodha hiyo, utukufu na fahari yao si pungufu kuliko ile ya jeshi la viumbe wengine wa mbinguni.

Kwa mapokeo, inasemekana kwamba Malaika Walinzi waliumbwa kwa kusudi moja tu la kutuhudumia katika mahitaji yetu. Ndiyo, Mungu angeweza kuchagua kututunza moja kwa moja bila kutumia malaika, lakini hakufanya hivyo. Alichagua kuwaumba malaika wawe wapatanishi wa neema na utunzaji Wake.

Ni sawa kusema kwamba Malaika wetu Walinzi wanatupenda kwa upendo mkamilifu. Wanatujua, wanatutunza na wanatamani sana tuwe watakatifu. Kusudi lao kuu ni kutufikisha Mbinguni na kutuvuta kwenye vilele vya utakatifu. Wanafanyaje hivyo?

Wanafanya hivyo kwa kutuletea neema ya Mungu. Neno โ€œmalaikaโ€ linamaanisha mjumbe. Hivyo, malaika wetu wana jukumu kuu la kutufahamisha mapenzi na mawazo ya Mungu. Wanaweza kusema yote ambayo Mungu anataka kutuambia. Pia ni walinzi, kwa kuwa wanaleta neema kutoka kwa Mungu katika hali maalumu za maisha ili kupambana na uovu na kutusaidia kutenda mema.

Tafakari leo juu ya zawadi ya malaika wako mlinzi. Kiumbe huyu wa mbinguni aliumbwa kwa kusudi moja tu la kukutunza na kukufikisha Mbinguni. Zungumza na malaika wako leo. Tegemea maombezi ya malaika wako na umruhusu malaika huyu mtakatifu akuletee neema tele ya Mungu.

Malaika wa Mungu, mlinzi wangu mpendwa, ambaye upendo wa Mungu umenikabidhi kwako hapa, uwe daima kando yangu leo, uniangazie na kunilinda, uniongoze na kunielekeza. Amina. Malaika wa Mungu, niombeeni. Yesu, nakutumainia.


Sala Yenye Nguvu Sana

Kumbukumbu ya Mama Yetu wa Rozari, Oktoba 7

Tunapomheshimu leo Mama Yetu wa Rozari, hii ni fursa nzuri ya kutafakari sala hii yenye nguvu. Njia bora ya kutafakari nguvu ya Rozari ni kuwasikiliza watakatifu. Hapa chini utapata kauli kadhaa za watakatifu wa Mungu kuhusu Rozari. Zitafakari na uziache ziseme na moyo wako.

โ€œKamwe hata mmoja anayesali Rozari yake kila siku hatapotoshwa. Hii ni kauli ambayo ningeisaini kwa furaha kwa damu yangu.โ€ – Mtakatifu Ludoviko wa Montfort.

โ€œKati ya sala zote, Rozari ndiyo nzuri zaidi na yenye neema nyingi zaidiโ€ฆipendeni Rozari na kuisali kila siku kwa ibada.โ€ – Mtakatifu Pio X.

โ€œNi nzuri jinsi gani familia inayosali Rozari kila jioni.โ€ – Mtakatifu Papa Yohane Paulo II.

โ€œRozari ndiyo sala ninayoipenda zaidi. Sala ya ajabu! Ya ajabu katika urahisi wake na kina chake.โ€ – Mtakatifu Papa Yohane Paulo II.

โ€œRozari ni hazina isiyokadirika thamani, iliyotokana na uvuvio wa Mungu.โ€ – Mtakatifu Ludoviko wa Montfort.

โ€œHakuna njia ya hakika zaidi ya kuomba baraka za Mungu zishukie familiaโ€ฆkuliko kusali Rozari kila siku.โ€ – Papa Pio XII.

โ€œRozari ndiyo aina bora kabisa ya sala na njia yenye nguvu zaidi ya kuufikia uzima wa milele. Ni dawa ya maovu yetu yote, mzizi wa baraka zetu zote. Hakuna njia bora zaidi ya kusali.โ€ – Mtakatifu Papa Leo XIII.

โ€œNipeni jeshi linalosali Rozari nami nitaushinda ulimwengu.โ€ – Mwenye Heri Papa Pio IX.

โ€œMkitamani amani mioyoni mwenu, katika nyumba zenu na katika nchi yenu, kusanyikeni kila jioni kusali Rozari. Msiache hata siku moja ipite bila kuisali, hata kama mmelemewa kiasi gani na mahangaiko na kazi nyingi.โ€ – Papa Pio XI.

โ€œMama Yetu hajawahi kuninyima neema kupitia kusali Rozari.โ€ – Mtakatifu Padre Pio.

โ€œNjia kuu zaidi ya kusali ni kusali Rozari.โ€ – Mtakatifu Fransisko wa Sales.

โ€œSiku moja, kwa njia ya Rozari na Skapulari, Mama Yetu atauokoa ulimwengu.โ€ – Mtakatifu Dominiko.

Bwana, nijalie kuelewa nguvu ya zawadi hii ya thamani, Rozari Takatifu. Nipe neema ya kuifanya sehemu ya sala yangu ya kila siku. Yesu, nakutumainia.


Kutumwa

Sikukuu ya Mtakatifu Luka, Mwinjili, Oktoba 18

โ€œMavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache; kwa hiyo mwombeni bwana wa mavuno atume watenda kazi kwa ajili ya mavuno yake. Enendeni zenu; tazama, ninawatuma kama wanakondoo kati ya mbwa mwitu.โ€ Luka 10:2-3

Leo tunamheshimu Mtakatifu Luka Mwinjili. Mtakatifu Luka aliandika mojawapo ya Injili nne, alikuwa mwenzi wa Mtakatifu Paulo ambaye alimpenda sana, alisafiri sehemu nyingi za mbali akihubiri Injili, na hatimaye akautoa uhai wake kama shahidi. Kwanza alifungwa gerezani kwa miaka miwili na, baada ya kuachiliwa, inasemekana kwamba alisulubiwa karibu na Akaya alipokuwa akiendelea na shughuli zake za kimisionari.

Mtakatifu Luka alikuwa mwenyeji wa Antiokia, jiji lililojulikana kwa utamaduni wake wa hali ya juu na elimu. Alikuwa tabibu, mwenye elimu nzuri na hadhi ya juu katika jamii. Hadhi yake katika jamii na elimu yake vinaonyesha kwamba alipitia ushahidi wa aina nyingine kabla ya kuuawa kwa ajili ya imani. Ushahidi alioupitia ulikuwa kuchagua Kristo badala ya umaarufu na heshima katika jamii.

Alipokutana na Injili, Mtakatifu Luka angeweza kwa urahisi kuuona utume aliopewa na Kristo kuwa jambo lililovuruga maisha yake ya starehe huko Antiokia.ย  Angeelewa haraka kwamba kuchagua kumfuata Bwana wetu na kukubali mwaliko wa kutumwa kuhubiri Injili kulihitaji kujitoa sadaka kwa kiasi kikubwa.ย  Hata hivyo, aliamua kuacha kila kitu ili kutimiza utume aliopewa na Bwana wetu.ย  Mungu alimtumia Mtakatifu Luka kwa njia nyingi, na hasa aliitumia elimu yake kama chombo ambacho kwa njia yake Roho Mtakatifu alimvuvia kuandika Neno la Mungu.

Kama Mtakatifu Luka, sisi sote tunaitwa na Mungu kumfuata bila kujibakiza na kutumwa katika utume wa pekee wa kutangaza Injili.ย  Kila wito ni tofauti, lakini kila wito lazima ukubaliwe kikamilifu na ufuatwe bila kuyumba.ย  Ni lazima tumtolee Kristo vipaji vyetu, mambo tunayoyapendelea, maisha yetu ya baadaye na maisha yetu yenyewe ili atutumie atakavyo.ย  Kumfuata Yesu daima kutahitaji namna fulani ya ushahidi wa kifodini, lakini namna yoyote ya ushahidi wa kifodini tunayoitwa kuikubali itazaa matunda mengi mema kwa ajili ya Ufalme wa Mbinguni.

Tafakari leo juu ya huyu mwanafunzi wa Bwana wetu mwenye akili na vipaji.ย  Furahia zawadi ambayo Mtakatifu Luka ametupatia katika Injili, lakini pia jitoe kumfuata Bwana wetu kwa kiwango kilekile alichomfuata mwanafunzi huyu.ย  Wewe, kama Mtakatifu Luka, unaitwa kuacha yote kwa ajili ya utume wa Injili.ย  Usisite kusema โ€œNdiyo.โ€

Bwana, tunapomheshimu huyu mwinjili mkuu, Mtakatifu Luka, nisaidie kuiga jinsi alivyojitoa kwa moyo wote kwa ajili ya Injili.ย  Unitumie, Bwana mpendwa, kama chombo cha Neno Lako Takatifu, na unipe ujasiri wa kuyatoa maisha yangu bila kujibakiza.ย  Yesu, nakutumainia.


Kusali Usiku Kucha

Sikukuu ya Watakatifu Simoni na Yuda, Mitume, Oktoba 28

Yesu alipanda mlimani kusali, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu.ย  Luka 6:12

Ni jambo la kuvutia kutafakari juu ya Yesu akisali usiku kucha.ย  Tendo hili Lake linatufundisha mambo mengi, kama ambavyo lingewafundisha Mitume Wake.ย  Haya ni baadhi ya mambo tunayoweza kujifunza kutokana na tendo Lake.

Kwanza, huenda mtu akafikiri kwamba Yesu โ€œhakuhitajiโ€ kusali.ย  Kwani, Yeye ni Mungu.ย  Je, basi alihitaji kusali?ย  Kwa kweli, hilo si swali sahihi la kuuliza.ย  Suala si kwamba alihitaji kusali, bali kwamba alisali kwa sababu sala Yake inagusa kiini cha Yeye ni nani.

Sala, kwanza kabisa, ni tendo la ushirika wa kina na Mungu.ย  Kwa Yesu, ni tendo la ushirika wa kina na Baba wa Mbinguni na Roho Mtakatifu.ย  Yesu alikuwa daima katika ushirika kamili (umoja) na Baba na Roho Mtakatifu, na hivyo sala Yake haikuwa kitu kingine ila udhihirisho wa ushirika huo hapa duniani.ย  Sala Yake ni kuudhihirisha kwa matendo upendo Wake kwa Baba na Roho Mtakatifu.ย  Kwa hiyo, si kwamba alihitaji kusali ili aendelee kuwa karibu Nao.ย  Badala yake, alisali kwa sababu alikuwa ameungana Nao kikamilifu.ย  Na ushirika huo kamili ulihitaji kudhihirishwa kwa sala hapa duniani.ย  Katika tukio hili, ilikuwa sala ya usiku kucha.

Pili, ukweli kwamba sala hiyo iliendelea usiku kucha unaonyesha kwamba โ€œpumzikoโ€ la Yesu halikuwa kitu kingine ila kuwa mbele ya Baba.ย  Kama vile pumziko linavyoturudishia nguvu na kutuchangamsha, ndivyo kukesha kwa Yesu usiku kucha kunavyoonyesha kwamba pumziko Lake la kibinadamu lilikuwa kupumzika mbele ya Baba.

Tatu, tunachopaswa kujifunza kutokana na hili kwa ajili ya maisha yetu wenyewe ni kwamba hatupaswi kamwe kudharau thamani ya sala.ย  Mara nyingi mno tunamwambia Mungu mawazo machache ya sala na kuishia hapo.ย  Lakini ikiwa Yesu alichagua kutumia usiku mzima katika sala, hatupaswi kushangaa ikiwa Mungu anataka mengi zaidi katika muda wetu wa sala ya utulivu kuliko yale tunayompa sasa.ย  Usishangae ikiwa Mungu anakuita kutumia muda mwingi zaidi katika sala kila siku.ย  Usisite kuweka utaratibu thabiti wa sala.ย  Na ukijikuta huwezi kulala usiku fulani, usisite kuamka, kupiga magoti na kutafuta uwepo wa Mungu anayeishi ndani ya nafsi yako.ย  Mtafute, msikilize, uwe pamoja Naye na umruhusu akutawale kabisa katika sala.ย  Yesu alitupa mfano mkamilifu.ย  Sasa ni wajibu wetu kuufuata mfano huo.

Tunapowaheshimu Mitume Simoni na Yuda, tafakari leo juu ya wito wako mwenyewe wa kumfuata Kristo na kutenda kama mtume Wake kwa ulimwengu.ย  Njia pekee unayoweza kuitumia kutimiza utume huu ni kuishi maisha ya sala.ย  Tafakari juu ya maisha yako ya sala, wala usisite kuimarisha azimio lako la kuiga kina na bidii ya mfano mkamilifu wa sala wa Bwana wetu.

Bwana Yesu, nisaidie kusali.ย  Nisaidie kufuata mfano Wako wa sala na kutafuta uwepo wa Baba kwa kina na daima.ย  Nisaidie kuingia katika ushirika wa kina Nawe na kutawaliwa kabisa na Roho Mtakatifu.ย  Yesu, nakutumainia.


Siku ya Watakatifu Wote!

Sherehe ya Watakatifu Wote, Novemba 1

Leo tunawaheshimu wanaume na wanawake watakatifu waliotutangulia katika imani, nao wamefanya hivyo kwa namna yenye utukufu.ย  Tunapowaheshimu hawa mashujaa wakuu wa imani, tutafakari wao ni nani na ni jukumu gani wanaloendelea kutimiza katika maisha ya Kanisa.ย  Dondoo lifuatalo limetoka katika Sura ya 8 ya Imani Yangu Katoliki!:ย ย 

Kanisa Linaloshinda:ย  Wale waliotutangulia na ambao sasa wanashiriki utukufu wa Mbinguni, wakimwona Mungu uso kwa uso, hawajatoweka.ย  Ni kweli kwamba hatuwaoni, wala si lazima tuweze kuwasikia wakizungumza nasi kwa namna ya kimwili kama walivyofanya walipokuwa duniani.ย  Lakini hawajatoweka hata kidogo.ย  Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu wa Lisieux alieleza jambo hili vizuri zaidi aliposema, โ€œNataka kutumia maisha yangu ya Mbinguni nikitenda mema duniani.โ€ย ย 

Watakatifu walioko Mbinguni wameungana kikamilifu na Mungu na ndio wanaounda ushirika wa watakatifu huko Mbinguni, yaani Kanisa Linaloshangilia!ย  Hata hivyo, jambo muhimu la kuzingatia ni kwamba, ingawa wanafurahia tuzo yao ya milele, bado wanatujali sana.

Watakatifu wa Mbinguni wamekabidhiwa jukumu muhimu la kutuombea.ย  Ni kweli kwamba Mungu tayari anajua mahitaji yetu yote, naye angeweza kutuomba tumwendee moja kwa moja katika sala zetu.ย  Lakini ukweli ni kwamba Mungu anataka kutumia maombezi ya watakatifu, na hivyo upatanishi wao, katika maisha yetu.ย  Anawatumia kupeleka sala zetu Kwake na, kwa upande mwingine, kutuletea neema Yake.ย  Wanakuwa waombezi wenye nguvu kwa ajili yetu na washiriki katika utendaji wa Mungu ulimwenguni.

Kwa nini hali iko hivi?ย  Tena, kwa nini Mungu hachagui tu kushughulika nasi moja kwa moja badala ya kupitia wapatanishi?ย  Kwa sababu Mungu anataka sisi sote tushiriki katika kazi Yake njema na katika mpango Wake wa kimungu.ย  Ni kama baba anayemnunulia mke wake mkufu mzuri.ย  Anawaonyesha watoto wake wadogo, nao wanafurahia zawadi hiyo.ย  Mama anaingia, naye baba anawaomba watoto wampelekee zawadi hiyo.ย  Zawadi hiyo inatoka kwa mume wake, lakini kuna uwezekano mkubwa kwamba atawashukuru kwanza watoto wake kwa kushiriki katika kumpa zawadi hiyo.ย  Baba alitaka watoto washiriki katika utoaji huo, naye mama alitaka watoto washiriki katika kuipokea zawadi na katika shukrani zake.ย  Ndivyo ilivyo kwa Mungu!ย  Mungu anataka watakatifu washiriki katika kugawa zawadi Zake nyingi za namna mbalimbali.ย  Na tendo hili linaujaza moyo Wake furaha!

Watakatifu pia wanatupa mfano wa utakatifu.ย  Mapendo waliyoishi duniani yanaendelea kuishi.ย  Ushuhuda wa upendo wao na kujitoa kwao haukuwa tendo la mara moja tu katika historia.ย  Bali mapendo yanaishi na yanaendelea kuleta matokeo mema.ย  Kwa hiyo, mapendo na ushuhuda wa watakatifu vinaendelea kuishi na kugusa maisha yetu.ย  Mapendo haya katika maisha yao yanajenga kifungo pamoja nasi, yaani ushirika.ย  Yanatuwezesha kuwapenda, kuwastaajabia na kutaka kufuata mfano wao.ย  Hili, pamoja na maombezi yao yanayoendelea, ndilo linalojenga kifungo imara cha upendo na umoja pamoja nasi.

Bwana, watakatifu wa Mbinguni wanapokuabudu milele, ninaomba maombezi yao.ย  Watakatifu wa Mungu, tafadhali njooni kunisaidia.ย  Niombeeni na mniletee neema ninayohitaji ili niishi maisha matakatifu kwa kuiga maisha yenu wenyewe.ย  Watakatifu wote wa Mungu, mtuombee.ย  Yesu, nakutumainia.


Roho Takatifu Zilizoko Toharani

Kumbukumbu ya Waamini Wote Waliotangulia Kufariki (Siku ya Wafu Wote), Novemba 2

Tunapoadhimisha Kumbukumbu ya Wafu Wote, tutafakari mafundisho ya Kanisa letu kuhusu Toharani. Dondoo lifuatalo limetoka katika Sura ya 8 ya Imani Yangu Katoliki!:ย ย 

Kanisa Linaloteseka:ย  Toharani ni fundisho la Kanisa letu ambalo mara nyingi halieleweki vizuri.ย  Toharani ni nini?ย  Je, ni mahali tunapopaswa kwenda ili kuadhibiwa kwa ajili ya dhambi zetu?ย  Je, ni njia ya Mungu ya kulipiza kisasi kwa mabaya tuliyofanya?ย  Je, ni matokeo ya hasira ya Mungu?ย  Hakuna swali lolote kati ya haya linalojibu kwa kweli swali la Toharani.ย  Toharani si kitu kingine bali ni upendo wa Mungu wetu unaowaka na kututakasa katika maisha yetu!

Mtu anapokufa akiwa katika neema ya Mungu, kuna uwezekano mkubwa kwamba hajaongoka kwa 100% wala hajawa mkamilifu katika kila jambo.ย  Hata watakatifu wakuu zaidi mara nyingi wangekuwa bado na upungufu fulani katika maisha yao.ย  Toharani si kitu kingine bali ni utakaso huo wa mwisho unaoondoa mifungo yote iliyobaki ya kushikamana na dhambi katika maisha yetu.ย  Kwa mfano wa kulinganisha, fikiria kwamba ulikuwa na kikombe cha maji safi kwa 100%, H2O safi.ย  Kikombe hiki kitawakilisha Mbingu.ย  Sasa fikiria kwamba unataka kuongeza maji katika kikombe hicho, lakini maji pekee uliyo nayo ni safi kwa 99%.ย  Haya yatawakilisha mtu mtakatifu anayekufa akiwa bado na mifungo michache tu midogo ya kushikamana na dhambi.ย  Ukiongeza maji hayo katika kikombe chako, basi maji yatakapochanganyika, kikombe kitakuwa sasa na angalau uchafu fulani ndani ya maji.ย  Tatizo ni kwamba Mbingu (kile kikombe cha awali cha H2O safi kwa 100%) haziwezi kuwa na uchafu wowote.ย  Katika mfano huu, Mbinguni hakuwezi kuwa na hata kifungo kidogo kabisa cha kushikamana na dhambi.ย  Kwa hiyo, ili maji haya mapya (maji safi kwa 99%) yaongezwe katika kikombe, lazima kwanza yatakaswe hata ile 1% ya mwisho ya uchafu (mifungo ya kushikamana na dhambi).ย  Ni bora zaidi hili lifanyike tukiwa bado duniani.ย  Huu ndio mchakato wa kuwa watakatifu.ย  Lakini tukifa tukiwa na kifungo chochote cha kushikamana na dhambi, basi tunasema tu kwamba mchakato wa kuingia katika kumwona Mungu Mbinguni kwa ukamilifu na milele utatutakasa na kuondoa kifungo chochote kilichobaki cha kushikamana na dhambi.ย  Huenda yote tayari yamesamehewa, lakini huenda hatujajinasua kutoka katika mambo hayo tuliyosamehewa.ย  Toharani ni mchakato, baada ya kifo, wa kuteketeza mifungo yetu ya mwisho ili tuweze kuingia Mbinguni tukiwa huru kwa 100% kutoka katika kila kitu kinachohusiana na dhambi.ย  Kwa mfano, ikiwa bado tuna tabia mbaya ya kukosa adabu au ya kusema kwa kejeli, hata mielekeo na tabia hizo lazima ziondolewe kwa utakaso.ย ย 

Hili hutokeaje?ย  Hatujui.ย  Tunachojua tu ni kwamba hutokea.ย  Lakini tunajua pia kwamba ni matokeo ya upendo wa Mungu usio na kikomo unaotuweka huru kutoka katika vifungo hivi.ย  Je, lina maumivu?ย  Yaelekea sana kuwa ndivyo.ย  Lakini lina maumivu kwa maana ya kwamba kuachana na kifungo chochote kisicho na mpangilio mwema huumiza.ย  Ni vigumu kuacha tabia mbaya.ย  Hata mchakato wenyewe una maumivu.ย  Lakini uhuru wa kweli unaopatikana mwishoni una thamani kuliko maumivu yoyote ambayo huenda tumepitia.ย  Kwa hiyo, ndiyo, Toharani kuna maumivu.ย  Lakini ni aina ya maumivu matamu tunayohitaji, na matokeo yake ya mwisho ni mtu kuungana na Mungu kwa 100%.

Sasa, kwa kuwa tunazungumzia ushirika wa watakatifu, tunataka pia kuhakikisha kwamba tunaelewa kuwa wale wanaopitia utakaso huu wa mwisho bado wako katika ushirika na Mungu, na wale washiriki wa Kanisa walio duniani, na wale walio Mbinguni. Kwa mfano, tumeitwa kuwaombea wale walio toharani. Sala zetu zina matokeo. Mungu hutumia sala hizo, ambazo ni matendo ya upendo wetu, kama vyombo vya neema Yake ya utakaso. Anaturuhusu na kutualika kushiriki katika utakaso wao wa mwisho kwa sala na sadaka zetu. Hilo hujenga kifungo cha umoja kati yetu na wao. Na bila shaka, watakatifu walio Mbinguni huwaombea hasa wale walio katika utakaso huu wa mwisho, huku wakingojea kuwa katika ushirika kamili nao Mbinguni. Ni wazo lenye utukufu, na ni furaha kuona jinsi Mungu alivyopanga mchakato huu wote kwa lengo kuu la ushirika mtakatifu ambao tumeitiwa!

Bwana, ninaziombea roho zile zinazopitia utakaso wao wa mwisho toharani. Tafadhali zimiminie huruma Yako ili ziwekwe huru kutokana na kila mshikamano na dhambi na hivyo ziwe tayari kukuona uso kwa uso. Yesu, nakutumainia.


Hasira ya Haki

Sikukuu ya Kuwekwa Wakfu kwa Basilika la Laterano huko Roma, Novemba 9

Yesu alipanda kwenda Yerusalemu. Katika eneo la hekalu aliwakuta watu waliokuwa wakiuza ngโ€™ombe, kondoo na njiwa, pamoja na wabadilishaji fedha waliokuwa wameketi hapo. Akatengeneza mjeledi wa kamba na kuwafukuza wote kutoka eneo la hekalu, pamoja na kondoo na ngโ€™ombe; akamwaga sarafu za wabadilishaji fedha na kupindua meza zao, na akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, โ€œOndoeni hivi hapa, na acheni kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa soko.โ€ Yohane 2:13b-16

Yesu alikasirika. Aliwafukuza wabadilishaji fedha kutoka hekaluni kwa mjeledi na kupindua meza zao huku akiwakemea. Bila shaka hilo lilikuwa tukio la kushangaza sana.

Jambo la msingi hapa ni kwamba lazima tuelewe Yesu alikuwa na โ€œhasiraโ€ ya aina gani. Kwa kawaida, tunapozungumzia hasira, tunamaanisha hisia kali ambayo imetushinda na, kwa kweli, inatutawala. Ni hali ya kushindwa kujitawala, nayo ni dhambi. Lakini hiyo si hasira aliyokuwa nayo Yesu.

Ni wazi kwamba Yesu alikuwa mkamilifu kwa kila namna, kwa hiyo tunapaswa kuwa waangalifu sana tusilinganishe hasira Yake na hasira tunayoipata kwa kawaida. Ndiyo, Kwake ilikuwa hisia kali, lakini ilikuwa tofauti na ile tunayoipata kwa kawaida. Hasira Yake ilitokana na upendo Wake mkamilifu.

Kwa Yesu, upendo kwa mwenye dhambi na hamu Yake ya kuona wenye dhambi wakitubu ndivyo vilivyochochea hisia Zake kali. Hasira Yake ilielekezwa kwenye dhambi waliyokuwa wamezama ndani yake, naye, kwa hiari na kwa makusudi, aliukabili uovu aliouona. Ndiyo, huenda jambo hilo liliwashtua wale waliolishuhudia, lakini katika hali hiyo, ilikuwa njia yenye matokeo bora zaidi ya kuwaita watubu.

Nyakati fulani tutatambua kwamba sisi pia tunapaswa kukasirishwa na dhambi. Lakini tuwe waangalifu! Ni rahisi sana kwetu kutumia mfano huu wa Yesu kuhalalisha kushindwa kujitawala na kuanguka katika dhambi ya hasira. Hasira ya haki, kama alivyoidhihirisha Yesu, daima itamwacha mtu akiwa na amani na upendo kwa wale wanaokemewa. Pia kutakuwa na utayari wa mara moja wa kusamehe pale majuto ya kweli kwa dhambi yanapoonekana.

Tafakari leo kuhusu hasira ya haki ambayo huenda Mungu akataka kuiweka moyoni mwako nyakati fulani. Tena, uwe mwangalifu kuitambua kwa usahihi. Usijiruhusu kudanganywa na hisia hii kali. Badala yake, ruhusu upendo wa Mungu kwa wengine uwe nguvu inayokusukuma, na uruhusu chuki takatifu dhidi ya dhambi ikuongoze kutenda kwa namna takatifu na ya haki.

Bwana, nisaidie kukuza moyoni mwangu hasira takatifu na ya haki ambayo unatamani niwe nayo. Nisaidie kutofautisha kilicho cha dhambi na kilicho cha haki. Hisia hii kali na hisia zangu zote zielekezwe daima katika kutimiza mapenzi Yako matakatifu. Yesu, nakutumainia.


Moyo Wenye Shukrani

Siku ya Kutoa Shukrani, Marekani

Yesu akajibu, โ€œWaliotakaswa walikuwa kumi, sivyo? Wale wengine tisa wako wapi? Je, hakuna aliyerudi kumpa Mungu shukrani isipokuwa huyu mgeni?โ€ Luka 17:17-18

Heri ya Siku ya Kutoa Shukrani! Ingawa Siku ya Kutoa Shukrani si hasa siku takatifu ya Kikatoliki, kwa hakika inaendana na maisha yetu ya imani. Kwa upande wa kiroho, sote tunajua kwamba shukrani ni kiini cha ujumbe wa Injili. Siku ya Kutoa Shukrani inatupatia fursa nzuri kabisa ya kutazama kipengele hiki mahususi cha imani yetu. Tumeitwa kuwa na shukrani za dhati milele. Una shukrani kwa Mungu kwa kadiri gani?

Huenda sisi sote tunapata ugumu kwa namna mbalimbali katika kuwa na shukrani. Ni sahihi kusema kwamba hatutawahi kuwa na shukrani za kutosha mpaka tutakapokamilishwa Mbinguni. Lakini kwa sasa, ni muhimu kutafakari kuhusu shukrani na kujitahidi kuziacha ziongezeke katika nafsi zetu.

Kwanza, hatutawahi kuwa na shukrani tusipoona wazi yote ambayo Mungu ametutendea. Katika maisha, ni rahisi sana kukazia macho magumu yote tunayokabiliana nayo na, kwa sababu hiyo, kuvunjika moyo, kuwa na huzuni nzito, kufadhaika na hata kukasirika nyakati fulani. Jambo lenye changamoto kubwa zaidi ni kutazama zaidi ya misalaba na mizigo tunayokabiliana nayo kila siku ili kuona wingi wa neema na huruma tunazopewa na Bwana wetu. Tusipoiona huruma na neema hiyo, tutapata ugumu mkubwa kuwa na shukrani za kweli.

Kwa hiyo, katika Siku hii ya Shukrani, tafakari swali hili rahisi: Je, ninayaona yote ambayo Mungu amenitendea? Je, ninaiona huruma Yake tele ikitenda kazi maishani mwangu? Kifungu cha Injili hapo juu kinaonyesha kwamba Yesu aliwaponya wakoma kumi, lakini mmoja tu kati yao alirudi kutoa shukrani. Je, wewe ni kama mmoja wa wale tisa walioshindwa kutoa shukrani? Ikiwa ndivyo, huenda unapata shida kuona baraka zote za kweli na tele kutoka kwa Mungu. Ukiweza kukiri kwa unyenyekevu kwamba unapata shida kuwa na shukrani kamili, utakuwa umepiga hatua ya kwanza ya kuona kwa uwazi zaidi na hatua ya kwanza ya kukuza shukrani za kina zaidi unazopaswa kuwa nazo. Kuwa na shukrani kunamaanisha kwamba unaiona kweli kwa uwazi. Uwe tayari kuipokea kweli hiyo, naye Mungu atayabadilisha maisha yako huku akikujaza furaha!

Bwana, tafadhali ujaze moyo wangu shukrani tele. Nisaidie kuelekeza macho yangu kwenye neema Yako na huruma Yako zisizo na kikomo. Nisaidie kuona zaidi ya mahangaiko ya maisha na mizigo inayonivunja moyo. Badala ya kukazia hayo, nisaidie kutambua zaidi na zaidi yote uliyonitendea na yote unayoendelea kunitendea. Yesu, nakutumainia.


Maandalizi ya Majilio

Sikukuu ya Mtakatifu Andrea, Mtume, Novemba 30

Yesu alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na ndugu yake Andrea, wakitupa wavu baharini; walikuwa wavuvi. Akawaambia, โ€œNifuateni, nami nitawafanya wavuvi wa watu.โ€ Mara moja wakaacha nyavu zao, wakamfuata. Mathayo 4:18-20

Ni sikukuu nzuri ajabu tunayoadhimisha leo tunapojiandaa kuanza kipindi chetu cha Majilio. Tunamheshimu Mtakatifu Andrea Mtume, anayetupa mfano kamili wa jinsi ya kuanza maadhimisho yetu ya Majilio yanayokuja.

Kifungu hiki hapo juu kinatufunulia mengi ya kutafakari. Andrea, pamoja na ndugu yake Petro, alikuwa mvuvi. Wavuvi hawa wawili walikuwa wakifanya kazi kwa bidii, wakati ghafla mtu huyu wasiyemjua, Yesu, alipopita karibu nao na kuwaita. Mara moja wakaacha kazi yao ya kujipatia riziki, wakamfuata Yesu.

Usikose kutambua kilichotokea hapa. Hasa, kuna mambo mawili yaliyotokea: 1) Yesu alipita karibu na wavuvi hawa wawili na kusema, โ€œNifuateni.โ€ 2) Kwa kuitikia, watu hawa wawili mara moja โ€œwaliacha nyavu zao na kumfuata.โ€

Simulizi hili la kuitwa kwa Mtakatifu Andrea linafaa sana kwa mwanzo wa Majilio, kwa sababu Majilio yanapaswa kuwa wakati ambapo Yesu anatuita upya. Yanapaswa kuwa mwanzo mpya na kuongoka upya kwetu. Majilio yanapoanza, tunapaswa kumsikia Yesu akituita, โ€œNifuateni!โ€ Tunapaswa kumsikia akitualika tujitoe kabisa kwa mpango na kusudi Lake la kimungu. Msikilize. Je, unamsikia akikuita?

Mwitikio wetu mwanzoni mwa Majilio unapaswa kuwa sawa na ule wa Mtakatifu Andrea. Tunapaswa, bila kusita, kuacha kila kitu ili kumfuata. Hilo linamaanisha nini hasa? Linamaanisha kwamba tunapaswa kuachana na chochote na kila kitu kinachotuzuia kumwitikia Kristo. Linamaanisha kwamba tunapaswa kuwa tayari na wenye nia ya kufanya chochote ambacho Yesu anatuomba. Na tunapaswa kuwa tayari kukifanya mara tu anapotuomba.

Tafakari leo ukweli kwamba Majilio ni wakati wa kuanza upya. Ni wakati wa kujiruhusu kuitwa kumwendea Kristo. Msikilize akikuita, nawe umwitikie kwa moyo wako wote.

Bwana, ninakupenda kuliko vitu vyote. Nisaidie kuisikia sauti Yako ya upole lakini thabiti ikiniita nikufuate. Unipe ujasiri ninaohitaji ili kuitikia mwaliko Wako wa upole kwa kujikabidhi Kwako kabisa. Majilio haya yawe wakati wa mwanzo mpya na wa azimio la dhati zaidi la kukufuata. Yesu, nakutumainia.

Yaliyomo


Pia Kinapatikana kama Kitabu chenye Jalada Laini & Kitabu cha Kielektroniki

Amazon.comย –ย Google Playย –ย iTunesย –ย Barnes and Noble

Shiriki ukurasa huu: