
Yesu mpendwa, katika Sakramenti ya Altare,
ushukuriwe na kusifiwa milele.
Upendo, unayestahili upendo wote wa mbinguni na duniani!
Wewe ambaye, kwa upendo usio na kikomo kwangu mimi,
mwenye dhambi asiye na shukrani,
ulitwaa asili yetu ya kibinadamu,
ukamwaga Damu Yako yenye thamani kuu ulipopigwa mijeledi kwa ukatili,
na ukakata roho juu ya Msalaba wa aibu kwa ajili ya heri yetu ya milele!
Sasa, nikiwa nimeangaziwa na imani hai,
nikimimina nafsi yangu yote na kwa ari ya moyo wangu,
ninakusihi kwa unyenyekevu,
kwa mastahili yasiyo na kikomo ya mateso Yako yenye uchungu,
unipe nguvu na ujasiri wa kuangamiza kila tamaa mbaya inayoutawala moyo wangu,
wa kukubariki kwa kutimiza wajibu wangu kwa ukamilifu,
kuchukia kabisa dhambi zote,
na hivyo kuwa mtakatifu.
Amina.