Ukweli Utawaweka Huru
Pakua kipindi: PDF – Toleo linaloweza kuhaririwa
Maandalizi Kabla ya Mkutano
Washiriki waombwe kusoma Sura ya Nane ya kitabu cha Maadili Yangu ya Kikatoliki! kabla ya mkutano huu.
Dakika 5 – Kukusanyika
Vitafunio na muda wa mazungumzo yasiyo rasmi watu wanapowasili. Jitahidini kuzingatia muda na kuwakusanya wote pamoja kabla ya kupita dakika 5 baada ya muda uliopangwa wa kuanza.
Dakika 5-10 – Sala ya kufungua na Maandiko Matakatifu
Wote wanaketi kimya wakati kiongozi anapoanza kwa Ishara ya Msalaba, kisha anawaalika kukaa kimya kwa muda kwa namna ifuatayo:
Tutulie tunapoanza kujifunza pamoja maadili yetu matukufu ya Kikatoliki. โBwana, tunapokaa hapa kimya kwa dakika moja, umsaidie kila mmoja wetu kuleta Kwako maswali yake mwenyewe, mahangaiko, hofu na furaha zake. Utusaidie, katika wakati huu wa ukimya, kuisikiliza kwa makini sauti Yako tulivu inayosema nasi, kutuongoza na kutuita tuwe na imani ya kina zaidi.โ
Kaeni kimya kwa takribani dakika moja mkiwa mmefumba macho ili kila mmoja aweze kuzungumza na Bwana wetu kuhusu mahangaiko na masuala yake binafsi yanayomtia wasiwasi.
Kiongozi anasoma mwaliko ufuatao:
Tulitafakari Neno la Mungu. Tutafakari safari yetu wenyewe ya imani kwa kujiuliza maswali yafuatayo: Je, ninaamini? Imani yangu ina kina gani? Je, niko tayari kumruhusu Mungu aseme nami? Je, niko tayari kulipokea Neno la Mungu na kuiruhusu kweli ya Mungu iingie ndani yangu kwa kina zaidi? Je, niko tayari kuruhusu imani hii mpya ibadilishe maisha yangu?
Kiongozi wa kipindi anasoma Maandiko Matakatifu yafuatayo kwa moyo wa sala, andiko moja baada ya jingine, akitua kwa takribani sekunde 30 kati ya mstari mmoja na mwingine:
Kutoka 20:16:ย Usimshuhudie jirani yako uongo.
Mathayo 5:33:ย โTena mmesikia kwamba waliambiwa wazee wenu, โUsiape uongo, bali mtimizie Bwana yote uliyoweka nadhiri.โ Lakini Mimi nawaambia, msiape kamweโฆโ
Yohane 14:5-6:ย Tomaso akamwambia, โBwana, hatujui unakokwenda; tutawezaje kuijua njia?โ Yesu akamwambia, โMimi ndimi njia na ukweliย na uzima. Hakuna anayekuja kwa Baba isipokuwa kwa njia Yangu.โย
Yohane 1:14:ย Naye Neno akawa mwili akakaa kati yetu, nasi tukauona utukufu Wake, utukufu wa Mwana wa pekee wa Baba, aliyejaa neema na ukweli.ย
Zaburi 119:163:ย Uongo nauchukia na kuukinai; sheria Yako naipenda.
Waefeso 4:29:ย Neno lolote chafu lisitoke vinywani mwenu, bali lile tu lililo jema kwa ajili ya kuwajenga wengine kadiri ya mahitaji yao, ili liwape neema wanaolisikia.
Zaburi 19:7:ย Sheria ya BWANA ni kamilifu, huiburudisha nafsi.ย Agizo la BWANA ni la kuaminika, huwapa hekima wasio na ujuzi.ย Maagizo ya BWANA ni ya haki, huufurahisha moyo.ย Amri ya BWANA ni wazi, huyatia macho nuru.
Kisha kiongozi anasema: Tukae kimya kwa muda, tukiyatafakari maneno haya. (dakika moja ya ukimya)ย ย
Kiongozi anawaalika wote kusikiliza sala ifuatayo na kuungana naye kimoyomoyo anaposali kwa sauti:
Bwana, Wewe ndiwe Ukweli, Njia na Uzima.ย Unisaidie kuishi kulingana na Neno Lako takatifu la Ukweli na kuishi kama unavyoniita niishi.
Uniepushe na udanganyifu, Bwana mpendwa, na unifanye kuwa mtu wa ukweli kwa kila namna.ย Unisaidie kuujua Ukweli, kuwekwa huru na Ukweli, na kuishi kikamilifu kulingana na Wewe uliye Ukweli.
Ninakukabidhi, Bwana mpendwa, mawazo yangu na maneno yangu, na kuyaweka wakfu Kwako.ย Mawazo matakatifu pekee yaingie akilini mwangu, na maneno Yako pekee yatoke kinywani mwangu.
Nisije kamwe nikapotoshwa na uongo na upotovu, bali niongozwe tu na yale yanayotoka katika fikra na mapenzi Yako.ย Ninakupenda, Bwana mpendwa.ย Yesu, nakutumainia.
Amina.
Muda wa sala unahitimishwa kwa wote kukiri Kanuni ya Imani ya Mitume:
Nasadiki kwa Mungu, Baba mwenyezi, Muumba mbingu na nchi; na kwa Yesu Kristo, Mwanawe pekee, Bwana wetu: aliyetungwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria; akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato, akasulubiwa, akafa, akazikwa. Akashuka kuzimu; siku ya tatu akafufuka katika wafu; akapaa mbinguni, ameketi kuume kwa Mungu Baba mwenyezi; kutoka huko atakuja kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, Kanisa takatifu katoliki, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa mwili, na uzima wa milele. Amina.
Dakika 45-50 – Maswali ya majadiliano
Kila mtu aalikwe kushiriki jambo au kuuliza swali akipenda, kuhusiana na maswali au vichocheo vya majadiliano vilivyo hapa chini.ย Jadilianeni swali moja baada ya jingine, na mpeni kila mtu nafasi ya kusema jambo akipenda.ย Epukeni kuruhusu mtu mmoja au wawili kutawala majadiliano.ย Mpeane nafasi kwa kufuata mduara, wala msiogope kushiriki mawazo yenu!ย Mawazo yenu yanaweza kumsaidia mtu mwingine kuelewa mada hizi.ย Huenda swali lako likawa ndilo swali alilo nalo mtu mwingine.ย Baadhi ya maswali yaliyo hapa chini yatawaalika kushiriki mambo ya maisha yenu wenyewe; mengine yatawaalika kushirikishana mliyosoma katika Sura ya Nane.ย Lengo ni kushiriki mambo ya maisha yetu wenyewe na kuhakikisha kwamba imani ya Kanisa letu inaelezwa kwa uwazi na kueleweka na wote.
- Amri ya Nane inatualika kufanya mambo mawili.ย Kwanza, inatuita kuepuka kusema uongo na kila aina ya udanganyifu.ย Pili, inatuita kuwa watu wanaoutafuta Ukweli kwa kina kabisa.ย Jadilianeni jinsi vipengele hivi viwili vya Amri hii vinavyoweka kiwango cha chini kinachotakiwa na pia kiwango cha juu cha kuitimiza Amri hii.
- Tumieni muda mfupi kujadili makosa yafuatayo dhidi ya Amri ya Nane:
- Kusema uongo moja kwa moja – Elezeni maana ya uongo wa moja kwa moja.ย Je, kuna wakati wowote ambapo inaruhusiwa kusema uongo?
- Kutoa ushahidi wa uongo chini ya kiapo – Ni nini kinachofanya kutoa ushahidi wa uongo chini ya kiapo kuwa kubaya zaidi kuliko kusema uongo moja kwa moja?ย Je, kuna wakati wowote ambapo mtu anaweza kutoa ushahidi wa uongo chini ya kiapo na kitendo hicho kikahesabiwa kuwa halali?
- Sifa njema ya wengine – Jadilianeni namna zifuatazo tunavyoharibu sifa njema ya mtu mwingine.ย Hili ni jambo linalotokea mara nyingi sana, hasa katika namba 1 na 2 hapa chini.ย Jadilianeni pia athari zake na namna mtu anavyopaswa kuitikia anapotendewa dhambi kwa njia hizi:
- Hukumu ya haraka – mtu anapochukulia kuwa ni kweli, bila msingi wa kutosha, kwamba jirani yake ana kosa la kimaadili, hata ikiwa anafanya hivyo kimoyomoyo tu
- Kuharibu sifa kwa kufichua makosa – mtu anapofichua makosa na mapungufu ya mwingine kwa watu ambao hawakuyajua, bila sababu yenye uhalali wa msingi
- Kusingiziaย – mtu anapoharibu sifa ya wengine kwa kauli zisizo za kweli na kutoa nafasi ya watu kuwahukumu kwa uongo
- Kujisifu – Kwa nini hili ni ukiukaji wa uaminifu kwa ukweli? ย Jadilianeni jambo hili, jinsi linavyofanana na kuharibu sifa kwa kufichua makosa, na jinsi lisivyo na unyenyekevu.
- Haki ya faragha – Jadilianeni umuhimu wa faragha na namna tunavyoweza kuheshimu zaidi faragha ya wengine.
- Siri za kitaalumaย – Toeni baadhi ya mifano hii iliyo wazi
- Vyombo vya habari – Tumieni muda wa kutosha kujadili vyombo vya habari. Mara nyingi vyombo vya habari vinakiuka uaminifu kwa ukweli kwa kutia chumvi, kuzingatia kupita kiasi mada moja, kuwasilisha mambo kwa upande mmoja, kuibua mihemko kwa habari za kusisimua, n.k. Mtakatifu angetendaje akiwa mwanahabari?
- Amri ya Nane inatuvuta kuelekea viwango vya juu kabisa. Jadilini vipengele vifuatavyo kuhusu kiwango cha juu kabisa cha uaminifu kwa ukweli:
- Kuingia katika Ukweli kamili wa Mungu – Ukweli hauishii tu katika kutofautisha kilicho kweli na kisicho kweli; bali ni kama bahari isiyo na kikomo cha kina wala upana wake. Jadilini njia ambazo mtu anaweza kuzama zaidi katika Ukweli.
- Uzuri kama Ukweli – Hii ina maana gani, na ukweli ni uzuri kwa namna gani? Je, uzuri โhutegemea mtazamo wa anayeutazama?โ Au uzuri una uhalisi wake wenyewe na unamtegemea Mungu?
- Sanaa kama kielelezo cha Ukweli – Sanaa huakisi na kushiriki katika ukweli kwa namna gani?
Dakika 20 – Tafakari za mwisho na kushirikishana
Mpeni kila mtu nafasi kwa zamu ya kushirikisha jambo ambalo huenda limemgusa zaidi katika majadiliano au lililomchanganya zaidi, ili apate ufafanuzi au uelewa zaidi kutoka kwa wengine.
Dakika 5 – Sala ya Kuhitimisha
Kiongozi anaanza kwa Ishara ya Msalaba na kuwaalika wote kukaa kimya kwa dakika moja, wakiwa wamefumba macho. Kila mtu atafakari yale yaliyojadiliwa, hasa jambo lililomgusa zaidi.
Kisha kiongozi anasali sala ifuatayo:
Tunakushukuru, Bwana mpendwa, kwa mazungumzo tuliyokuwa nayo kuhusu Wewe na Ukweli unaotoka katika akili na moyo Wako. Utujalie neema, kila siku bila kukosa, ya kuzama katika yote uliyofundisha na kufunua.
Utusamehe, Bwana mpendwa, kwa namna tulivyokiuka Ukweli katika maisha yetu, na uturudishe katika neema Yako. Tunaomba msamaha kwa madhara ambayo maneno na mawazo yetu yamewaletea wengine, na neema ya kuleta uponyaji na amani.
Uukomboe ulimwengu wetu kutoka katika upotovu na dhambi, na uiimarishe sheria Yako ili itawale katika jamii kwa kila namna.
Yesu, nakutumainia.
Kisha kiongozi anawaalika wote waliopo kutoa sala zao wenyewe kwa namna ifuatayo (Angalizo: Hili linaweza kufanywa kwa sauti, lakini huenda ikafaa zaidi lifanywe kimya kimya, kadiri kiongozi atakavyoona inafaa):
Sasa kila mmoja wetu alete mahangaiko yake binafsi mbele ya Bwana wetu, akitumaini kwamba Yeye anatusikia na anajua yote tunayohitaji.ย Tumkabidhi sala hizi tukiwa na tumaini kamili kwamba anatamani kushika usukani.
(Kaeni kimya kwa dakika moja ili kila mtu azungumze na Mungu kuhusu mahitaji yake binafsi ya usiku huo).
Kisha kiongozi anawaalika wote kuhitimisha kwa sala za Baba Yetu, Salamu Maria na Atukuzwe Baba.
Yaliyomo katika Vipindi vya Mafunzo
