Kiswahili

Rozari ya Maandiko Matakatifu

“Picha ya kimapokeo ya Mama Yetu wa Rozari humwonyesha Maria akiwa amembeba mtoto Yesu mkononi mwake na akimkabidhi rozari Mtakatifu Dominiko. Taswira hii yenye maana kubwa inaonyesha kwamba rozari ni njia tuliyopewa na Bikira Maria ya kumtafakari Yesu na, kwa kutafakari maisha Yake, kumpenda na kumfuata daima kwa uaminifu unaozidi kukua.” Benedikto XVI

Nukuu za Watakatifu kuhusu Rozari Takatifu

Tazama pia: Tafakari za Rozari
kutoka Kupanda Ngazi za Mbinguni

Rozari ni sala inayotegemea Maandiko Matakatifu. Huanza na Kanuni ya Imani ya Mitume, ambayo hufupisha mafumbo makuu ya imani Katoliki. Baba Yetu, inayotangulia kila fumbo, imetoka katika Injili. Sehemu ya kwanza ya Salamu Maria ni maneno ya malaika anayetangaza kuzaliwa kwa Kristo na salamu ya Elisabeti kwa Maria. Mtakatifu Pio V aliongeza rasmi sehemu ya pili ya Salamu Maria. Mafumbo ya Rozari yanahusu matukio ya maisha ya Kristo. Kuna makundi manne ya Mafumbo: ya Furaha, ya Uchungu, ya Utukufu na––yaliyoongezwa na Papa Yohane Paulo II mwaka 2002––ya Mwanga.

Kurudiarudia maneno katika Rozari kunakusudiwa kumwongoza mtu katika sala yenye utulivu na tafakari inayohusiana na kila Fumbo. Kurudiarudia maneno kwa upole hutusaidia kuingia katika ukimya wa mioyo yetu, ambamo roho ya Kristo hukaa. Rozari inaweza kusaliwa faraghani au pamoja na kikundi.


Chagua Mafumbo

Chagua Mafumbo unayotaka kusali. Kila ukurasa una masomo ya Maandiko Matakatifu, sala za Rozari, na rekodi ya sauti.

Mafumbo Matano ya Furaha

Kwa mapokeo husaliwa Jumatatu, Jumamosi, na Jumapili za Majilio.

Sali Mafumbo ya Furaha →

Mafumbo Matano ya Mwanga

Kwa mapokeo husaliwa Alhamisi.

Sali Mafumbo ya Mwanga →

Mafumbo Matano ya Uchungu

Kwa mapokeo husaliwa Jumanne, Ijumaa, na Jumapili za Kwaresima.

Sali Mafumbo ya Uchungu →

Mafumbo Matano ya Utukufu

Kwa mapokeo husaliwa Jumatano na Jumapili zisizo katika nyakati za Kwaresima na Majilio.

Sali Mafumbo ya Utukufu →


Kusali Rozari

Jifunze na/au saidia kikundi chako kujifunza sala za Rozari.

  1. Fanya Ishara ya Msalaba.
  2. Ukiwa umeshika msalaba wenye sanamu ya Yesu, sali Nasadiki ya Mitume.
  3. Kwenye ushanga wa kwanza, sali Baba Yetu.
  4. Sali Salamu Maria moja kwenye kila ushanga kati ya shanga tatu zinazofuata.
  5. Sali Atukuzwe Baba.
Kusali Mafumbo
  1. Kwa kila fungu kati ya mafungu matano ya Rozari, tangaza Fumbo (ukipenda, unaweza kufuatisha somo la Maandiko Matakatifu lililotolewa kwenye ukurasa wa fumbo husika hapo juu), kisha sali Baba Yetu.
  2. Ukishika kwa vidole kila ushanga kati ya shanga kumi zinazofuata, sali Salamu Maria kumi huku ukitafakari Fumbo.
  3. Kisha sali Atukuzwe Baba.
  4. Baada ya kumaliza kila fungu la Rozari, baadhi ya watu husali sala ifuatayo iliyoombwa na Bikira Maria Mbarikiwa huko Fatima:
    Ee Yesu wangu, utusamehe dhambi zetu, utuokoe na moto wa Jehanamu; uziongoze roho zote Mbinguni, hasa zile zinazohitaji zaidi huruma Yako.

Baada ya kusali mafungu matano, sali:

  1. Salamu, Malkia Mtakatifu
  2. Kwa hiari: sala ya kuhitimisha
  3. Kwa hiari: Sala ya Mtakatifu Mikaeli
  4. Kwa hiari: Sala kwa Mtakatifu Yosefu
  5. Kwa hiari: Sala Zilizotoholewa kutoka kwa Papa Fransisko kwa Nyakati za Mateso


Sehemu kubwa ya maandishi na picha ya Rozari vimechukuliwa kutoka kwenye ukurasa wa tovuti wa Maaskofu wa Marekani: Jinsi ya Kusali Rozari.

Asanteni maaskofu na wafanyakazi wa USCCB! Tunawaombea!


Sala Zaidi
Tafakari za Kila Siku

Shiriki ukurasa huu: