Kiswahili

MAUMIVU YAKO YATAKUWEKA HURU

Mateso huleta thawabu ya maisha.
Acha mateso yakufungulie njia ya kuja Kwangu.
Yaache yaioshe nafsi yako.
Yaache yaiweke huru roho yako.

Mateso yanahitajika ili kupata mwanga wa ufahamu.
Yataufungua moyo wako.
Yatakufungua macho.
Yatakuweka huru.

Acha mateso yako yalete matumaini.
Acha mateso yako yatoe hekima.
Acha mateso yako yafuate mpango Wangu
  na yaishie katika amani na furaha yenye utulivu.

Akili yako isiteswe na mahangaiko.
Ruhusu tu maumivu yako yatumiwe.
Uwe na amani katika maumivu yako,
  yanapokuongoza kwenye nchi Yangu.
Nijongee kwa moyo wako,
  kwa kuwa mwelekeo huu ni wako.
Nikabidhi maumivu yako, kwa maana nitakuweka huru.

Tafakari Inayofuata

Yaliyomo

Shiriki ukurasa huu: