Kiswahili

Sala ya Kipindi cha Pasaka


Aleluya! ย Bwana Yesu, umefufuka kutoka kwa wafu na umeshinda kwa utukufu!

Bwana, nakushukuru kwa dhati kwa kuwa ninaweza kujiunga katika sherehe ya Ufufuko Wako! ย Nakushukuru kwa kunipenda sana hata nimealikwa kushiriki katika uzima mpya ulioupata kwa ushindi Wako.

Bwana mpendwa, njia ya kuelekea Ufufuko ilikuwa ya maumivu na mateso makubwa sana. ย Ilikutaka kuyatoa maisha Yako yote kuwa sadaka. ย Hukubakiza kitu chochote, bali uliyatoa maisha Yako hadi tone la mwisho la damu.

Bwana Mfufuka, ujumbe wa furaha ni kwamba mateso na kifo havikuwa mwisho. ย Ulifufuka kwa ushindi katika mwili mpya uliotukuzwa, ukiwafungulia mlango wote wanaokuamini ili nao wafufuke vivyo hivyo. ย Bwana mpendwa, nivute nishiriki katika mateso na kifo Chako ili pia nivutwe kushiriki katika utukufu wa Ufufuko Wako. ย Nipe ujasiri uliokuwa nao ulipovumilia mateso mengi namna hiyo. ย Nisaidie kukabiliana na misalaba ya maisha yangu kwa nguvu Zako. ย Ninapofanya hivyo, nijaze matumaini huku nikitarajia uzima mpya utakaouleta kutokana na mateso yote yanayounganishwa na Wewe.

Aleluya! ย Bwana Yesu, umefufuka kutoka kwa wafu na umeshinda kwa utukufu!

Aleluya! ย Utukufu na sifa zote ni Kwako, Bwana mpendwa, kwa ajili ya Ufufuko Wako!

Aleluya! ย Utukufu wa Ufufuko Wako na upendwe, upokelewe kwa moyo wote na kutangazwa mpaka mwisho wa nyakati na hata milele!

Shiriki ukurasa huu: